GET /api/v0.1/hansard/entries/400767/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 400767,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/400767/?format=api",
"text_counter": 67,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Boy Juma Boy",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 758,
"legal_name": "Boy Juma Boy",
"slug": "boy-juma-boy"
},
"content": "Bw. Spika, majina yalipoletwa hapa hayakuwa na tatizo. Hoja ilipita na kupelekwa mbele bila matatizo yoyote. Sasa tunakubaliana na uamuzi wa Spika, lakini cha msingi hapa ni kwamba ni uamuzi wa Seneti ndio uliopingwa kule na wala sio uamuzi wa chama. Kwa hivyo, kinachojadiliwa hapa sio nani apate nini bali kinajulikana kinagaubaga. Kama hutaki kulielewa hilo jambo basi itabaki hivyo, lakini anayeona na macho na kusikia kwa masikio, ni kwamba Seneti ilikuwa imemaliza mambo haya. Asante, Bw. Spika."
}