GET /api/v0.1/hansard/entries/401454/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 401454,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/401454/?format=api",
"text_counter": 169,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Muthama",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 96,
"legal_name": "Johnson Nduya Muthama",
"slug": "johnson-muthama"
},
"content": "Bw. Naibu Spika, nasimama kuunga mkono Hoja hii. Kama kungekuwa na usawa, hata hatungeongea sana na kusema kwamba tunauliza Serikali ama kaunti ziangalie masuala ya waalimu ambao watafundisha watoto wetu wachanga ambao ndio wanaanza elimu ya msingi. Lakini ingekuwa jambo la kawaida na la haki kuhakikisha kwamba Serikali kuu inazingatia masilahi ya walimu wa elimu ya chekechea ili kuhakikisha kwamba pale pahali walimu wa zile sehemu zingine walipowekwa, vile vile walimu hawa wamewekwa pale. Bw. Naibu Spika, ni jambo la kuhuzunisha sana kuona kwamba Wakenya fulani wanaishi maisha ya kubahatisha katika taifa lao. Wakenya ni wale wanaosomesha shule za chekechea. Bw. Naibu Spika, walimu hawa hulipwa na pesa zinazochangwa na wazazi. Jambo hili hufanyika kote nchini. Hawa wazazi wenyewe hawana pesa, ni masikini sana. Wao huchanga ili watoto wao wapate elimu ya chekechea, Utakuta kwamba yule anayefundisha katika shule hizi za chekechea mara nyingi anapata Kshs1,000, Kshs1,500, Kshs2,000. Wakati mwingine pesa hizi hazipatikani kabisa. Jambo hili linakuwa ni kama la msaada ilhali tunafahamu kwamba mtoto akitayarishwa vilivyo katika msingi wa kudumu kutoka shule za chekechea halafu aende katika shule ya msingi akiwa amejihami na kujimudu vizuri, yeye huelewa masomo ya msingi kwa urahisi sana. Ikiwa ataenda bila ya kujimudu, basi itakuwa ni vigumu kwake kuelewa na masomo ya msingi. Kwa hivyo, ni jukumu la Serikali kuu kujua kwamba Kenya ni yetu sisi sote na tunagawanya raslimali zetu katika viwango vyote. Ni lazima tuhakikishe kuwa raslimali kutoka Serikali kuu zinawafikia watu wetu kule mashinani. Hii ndio njia moja ya watu wetu kujivunia nchi yao na Serikali yetu. Bw. Naibu Spika, tunapozungumzia mambo ya elimu ya watoto wetu, hatulengi tu watu wa daraja fulani katika maisha. Tunajua kwamba watoto au watu wengi ambao wamefaulu katika maisha wanatoka katika daraja ya chini au ni watoto wa watu masikini. Hawa ndio wanaohitaji kusaidiwa na Serikali kuu. Lakini tukiangalia vile mambo The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate"
}