GET /api/v0.1/hansard/entries/401456/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 401456,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/401456/?format=api",
    "text_counter": 171,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "yalivyo hivi sasa, ni watoto wa matajiri kama vile Sen. (Dr.) Khalwale, Sen. Muthama, Sen. Mositet na wale wengine ambao watafaidika. Je, watoto wa masikini wataendelea lini? Watoto wa hawa matajiri wataendelea kutawala na kufaulu hadi mwisho wa dunia. Kwa hivyo, ili tuinuke pamoja na tuendelea pamoja, ni lazima Serikali kuu na za kaunti zifanye kazi pamoja. Mambo haya yasije kuwachiwa serikali za kaunti pekee. Serikali haiwezi kuwa inatoa lile jukumu lake la kufanya kazi na sisi tunakuja tu hapa kusema “kaunti ifanye hii; Serikali itoe pesa iwaajiri walimu wa shule za chekechea. Wawalipwe mishahara kiasi hiki na hiki. Jukumu lao haliishi pale wanapowaajiri walimu. Mara nyingi shule za chekechea huwa na mwalimu mmoja. Mwalimu huyo ikiwa mgonjwa, basi siku hiyo au wiki hiyo, hakuna masomo. Watoto katika shule hizo husomea katika mazingira mabaya sana. Wao hukekiti kwa mawe. Hawana chakula wala maji. Naona kuwa nchi hii haitafika mahali popote kimaendeleo ikiwa masomo ya shule za chekechea hayatazingatiwa kwa makini. Hii ni kwa sababu masomo haya huweka msingi maalum kwa watoto wetu. Viongozi wazuri watatoka katika shule hizi. Kwa hivyo, ni lazima wawe na msingi thabiti. Tukifanya hivyo, Mungu aliye juu atatubariki na nchi yetu itaenda mbele. Tutaweza kuinua maisha ya masikini wengi katika nchi hii na katika familia zao tunaweza kupata marubani wa ndege, daktari, walimu na wengine wengi. Mama akizaa mtoto, si tu anaona watoto wa Sen. Muthama wanapita wakienda ile shule nzuri ilhali watoto wake wanaenda katika shule iliyochakaa pale. Ni jukumu langu kuhakikisha kwamba kama kiongozi katika Serikali, shule anayoenda mtoto wa masikini inafanana na ile anayosomea mtoto wangu. Bw. Naibu Spika, jambo linaloendelea nchi hii ni jambo la kuleta kizaazaa cha mauti siku moja kwa sababu ya hiyo tabia tuliyoiga tangu tujinyakulie Uhuru. Unapoishi wewe na ninapoishi mimi hapa Nairobi ni kama tunaishi ndani ya jela. Milango ya nyumba zetu ni ya chuma. Mlango wa nje wa nyumba yako ni wa chuma, mlango wa ndani ni wa chuma, dirisha ni ya chuma na kadhalika. Ikiwa nyumba hiyo kwa bahati mbaya itashika moto, basi hakuna mali au mtu atakayeokolewa. Hakuna nafasi ya kujiokoa. Utaumia pale ukitafuta ufunguo za kufungua zile kufuli. Kilichosababisha mambo haya ni nini? Ni Kenya kuwa na matajiri 10 ilhali wananchi milioni arubaini wakiwa masikini. Na kama tutaendelea hivyo, basi kila tunachofanya tutaambulia patupu. Siku moja tutakuja kuporomoka kama nyumba ya matope au ya makaratasi. Kwa hayo machache, Bw. Naibu Spika, naomba kuunga mkono Hoja hii."
}