GET /api/v0.1/hansard/entries/401461/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 401461,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/401461/?format=api",
"text_counter": 176,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Chelule",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13126,
"legal_name": "Liza Chelule",
"slug": "liza-chelule"
},
"content": "Asante, Bw. Naibu Spika, kwa kunipa fursa hii ili nichangie Hoja ya leo iliyoletwa na Sen. Karaba kuhusu watoto wetu wachanga. Naunga mkono Hoja hii ili watoto wetu wachanga wapate msingi bora; pia yatakikana sisi, kama viongozi, tuwaangalie vizuri watoto wetu wachanga. Nimeketi na kufikiria ni kwa nini Serikali peke yake imelenga shule za msingi ama vyuo ambavyo walimu wanaofunza madarasa ya juu wanafuzu, ilhali shule za chekechea zimepuuzwa. Nafikiri itakuwa jambo la maana sana iwapo sisi, kama viongozi wa nchi hii, tutaangalia msingi bora wa watoto wetu kwa sababu hapo ndipo mambo yote yanapoanza. Bw. Naibu Spika, kuna ripoti moja iliyochapishwa iliyosema kwamba kuna watoto walioko madarasa ya sita ama saba ambao hawawezi kusoma wala kuandika. Hili linafanyika kwa sababu msingi wao haukukamilika. Nasema hivi kwa sababu madarasa ya watoto wachanga yanafaa kuwa tofauti na yale madarasa mengine ya watoto wakubwa. Madarasa haya yanafaa yawe spesheli. Walimu wao lazima waangaliwe na wapewe mafunzo na elimu ya kutosha ili wawaangalie watoto wetu wachanga kwa makini. Mahitaji ya watoto wadogo si masomo peke, bali ni lazima tuzingatie mambo ya afya yao, vyakula na madarasa wanayosomea. Mambo haya yote ni lazima yaangaliwe kwa makini sana iliwaweze kujikimu katika maisha yao ya kimasomo. Bw. Naibu Spika, Sen. Karaba ameangalia mambo haya kwa makini sana. Nataka kuwaunga mkono Maseneta wenzangu kwa kusema kuwa lazima tubuni mikakati au sera ambazo zitafuatiliwa na kutekelezwa na serikali za kaunti. Lazima tuangalie ni nani atachaguliwa aende kufunzwa kuhusu mambo ya watoto wadogo. Ni lazima tuangalie watu hawa watachaguliwa aje, wataajiriwa kazi kwa njia gani. Kwa hivyo, kama Seneta, nina hakika kuwa Maseneta wako na nguvu na uwezo wa kutekeleza sera nzuri kama hii ambayo itatekelezwa na serikali za kaunti. Bw. Naibu Spika, kwa sababu Hoja hii ni ya maana sana, ningeomba ipitishwe na kutekelezwa kwa haraka iwezekanavyo. Kwa hayo machache, naomba kuunga mkono Hoja hii."
}