GET /api/v0.1/hansard/entries/403572/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 403572,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/403572/?format=api",
"text_counter": 359,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Khamisi",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 874,
"legal_name": "Mishi Juma Khamisi",
"slug": "mishi-juma-khamisi"
},
"content": "Bw. Naibu Spika wa Muda, nimesimama kuupinga Mswada huu kwa sababu ingawaje ni Mswada mzuri, unatashiwishi. Waswahili wanasema hata unapopika mchuzi wako mzuri, unapoingia jongoo hauwezi kuwa mzuri. Kama Wakenya, tunatambua kwamba tumekuwa katika mapambano makali sana kuhakikisha kwamba kumekuwa na uhuru wa habari na kuvipatia vyombo vya habari uhuru na kupata uhuru wa kujieleza. Katiba yetu, katika Sura ya Nne, Vipengele 33, 34 na 35, inazungumzia jinsi tulivyopata uhuru wa kujieleza, uhuru wa vyombo vya habari na uhuru wa kupata habari katika nchi yetu. Kwenye Mswada huu, kuna Kipengele kinachosema kwamba kutakuwa na Tume itakayopokea malalamiko. Tume hiyo imepewa nguvu nyingi, ambazo zinaweza kumfanya mwanahabari asiweze kufanya kazi yake."
}