GET /api/v0.1/hansard/entries/403579/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 403579,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/403579/?format=api",
"text_counter": 366,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Khamisi",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 874,
"legal_name": "Mishi Juma Khamisi",
"slug": "mishi-juma-khamisi"
},
"content": "Jopo lililopendekezwa kwenya Mswada huu ili kuangalia nidhamu ya wanahabari ni jopo ambalo nguvu zake ni nyingi mno kiasi cha kwamba mwanahabari anaweza kupokonywa kibali cha kazi yake, na taasisi za uanahabari pia kupokonywa vibali vya kufanyia kazi na akaunti zao kwenye mabenki kufungwa na kuambiwa wasiendelee na kazi yao. Hili ni jambo ambalo halitaweza kukubalika. Cha msingi ni kuweza kuangalia na kupima uanahabari ulio na nidhamu na uanahabari usio na nidhamu na wenye kutumia nguvu. Naibu Spika wa Muda, pengine ningezungumza kwa Kingereza ili wenzangu ambao hawaelewi lugha sanifu ya Kiswahili, waweze kuelewa. We need to address media so that there is a balance between aggressive reporting and responsible journalism. Hilo ndilo jambo ambalo linaleta utata katika Kenya kwa sababu wanahabari wengi ni wale ambao hawana taaluma ya uanahabari mwafaka. Hivyo basi, wanatoa habari ambazo zina uchochezi ama zinapita mipaka ya kisheria. Lakini tunapofuata njia sawa, tutaweza kuwa na habari sawa. Wakenya wenzangu, lazima tutambue kwamba Kenya tuko miongoni mwa nchi ambazo zimesifika kwa kulinda haki za wanahabari. Ndio sababu katika nchi kama Ethiopia na Eritrea kuna wanahabari wengine ambao wamekimbilia Kenya ili kuja mafichoni na kupata afueni. Naibu Spika wa Muda, ikiwa tutaweka sheria ambazo tutampatia Waziri nguvu nyingi katika baraza hili la wanahabari, basi tutarudi katika zile siku za giza; siku ambazo habari zitakuwa si sawa. Mfano mzuri ni juzi katika nchi yetu ya Kenya. Wanahabari wetu walitupatia matukio muhimu sana; matokeo ya uchaguzi wetu mkubwa, matukio ya uvamizi katika soko la Westgate ambayo ni mambo ya kigaidi na pia habari kuhusu kesi inayoendelea katika Korti la Kimataifa, ICC. Iwapo jambo hili la wanahabari litakuwa chini ya himaya ya Waziri ambaye amekula kiapo kulinda Serikali yake, basi mambo mengi kuhusu kupata habari hayatakuwa sawasawa. Walalahoi Wakenya maskini hawangejua yaliyojiri katika soko la Westgate kama nguvu zote nyingi zitakuwa zimepelekwa katika ofisi ya Waziri. Tunaona hata lile jopo, Bw. Waziri ndiye atatengeneza. Naibu Spika wa Muda, hata lile jopo la rufaa, ambalo kwa Kingereza tunaliita"
}