GET /api/v0.1/hansard/entries/403665/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 403665,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/403665/?format=api",
    "text_counter": 76,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. (Dr.) Machage",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 179,
        "legal_name": "Wilfred Gisuka Machage",
        "slug": "wilfred-machage"
    },
    "content": "Nakushukuru sana, Bw. Spika wa Muda. Wazo hili la Sen. Liza la kuleta maendeleo katika taifa la Kenya limekuja wakati ufaao. Bw. Spika wa Muda, Sen. Liza ameangazia mawazo yake kwa hili shirika la fedha la kilimo ambalo linajulikana kama AFC. Naomba kwamba riba ambayo shirika hili linawatoza wakulima ya asilimia 10 ipunguzwe hadi asilimia tatu. Kwa kufanya hivyo, shirika hili litakuwa likiangazia mawazo yake kwa shida za wakulima. Tunajua kwamba tangu Uhuru, miaka karibu 50 iliyopita, kumekuwa na mambo ya kunyanyasa wakulima kila wakati. Kuna utumwa mamboleo kwa sababu mambo yao ni kufanya kazi lakini hawaoni yale ambayo wanafanyia kazi. Hii ni kwa sababu ya riba kubwa inayotozwa mikopo na shirika hili. Kama ni kuuza mazao, mara nyinigi hakuna soko au wanauza kwa bei duni. Wakati mwingi hata nafaka zao huchukuliwa bila malipo na mashirika ambayo yanajifanya kuwa yamefilisika. Nina mfano wa kampuni kama Mastermind ambayo huchukua mazao ya tumbaku kutoka sehemu za Nyanza kusini, ikijidai kwamba inaweza kulipa. Hata hivyo, wanakaa na mazao hayo miaka nenda, miaka rudi, bila kulipa. Jambo hili ni lazima likataliwe kabisa. Bw. Spika wa Muda, Maseneta hupewa mikopo na Serikali kwa ajili ya ujenzi wa nyumba zao na hata kununua magari ya kifahari kwa riba ya asilimia tatu tu. Hivi majuzi, Bi. Sara Serem, alikubali kwamba wabunge wa kaunti pia wapewe mikopo ya Kshs3 milioni kwa ajili ya kununua vitu kama vile nilivyotaja kwa riba ya asilimia tatu. Kwa hivyo, inawezekana kutoa riba ya asilimia tatu kwa wananchi wa Kenya. Swali ni: Je, wananchi wote wa Kenya ni sawa? Kama wananchi wote wa Kenya ni sawa kwani wale ambao wako uongozini wanapewe mikopo kwa riba ndogo ilhali wakulima ambao pia ni wapiga kura, bado wanaendelea kunyanyaswa kwa riba ya asilimia 10? Huu ni unyanyasaji. Bw. Spika wa Muda, wale watega uchumi wakubwa au mabwenyenye wanataka mkulima mdogo apewe mkopo kwa riba ya asilimia 10 halafu ashindwe kulipa. Huyo The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate"
}