GET /api/v0.1/hansard/entries/403667/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 403667,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/403667/?format=api",
    "text_counter": 78,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "bwanyenye atafanya kila jambo kuhakikisha kuwa amelinunua shamba hilo la maskini hohehahe kwa bei ya chini. Ukweli ni lazima usemwe. Siku moja nikienda kaburini ni lazima watu wetu wakumbuke kwamba Sen. (Dr,) Machage alikuwa anasema ukweli. Majuto ni mjukuu; huja baadaye. Bw. Spika wa Muda, sisemi tu riba ipunguzwe bali hata wale walioshindwa kulipa mikopo miaka mingi iliyopita wasamehewe na mikopo hiyo ifutiliwe mbali. Naipongeza Serikali kwa kujitolea na kuangaza mawazo yake kwa wale walioathirika kutokana na vita vya 2007. Juzi walipewa Kshs400,000 kila mtu na zingine Kshs10,000 za kuhama. Je, kuna tofauti gani kati ya yule Mkenya ambaye aliathirika mwaka wa 2007 na yule aliyeathirika kwa kushindwa kulipa mkopo kwa sababu ya riba ya juu, jua kali na hakuweza kuvuna mazao yoyote? Yeye analia na kusononeka na watoto hawawezi kusoma. Hata hivyo, anaachwa bila kuangaliwa na Serikali yetu. Je, kuna tofauti gani ilhali lile pia ni janga kubwa? Janga la hivi majuzi lilikuwa la kujitakia. Bw. Spika wa Muda, hata stakabadhi ambazo zinawekwa na Serikali hutupwa baada ya miaka 30. Zingine ambazo zilikuwa za siri hutolewa ili watu wasome kile kilichotendeka. Kwa sababu miaka 30 mambo mengi yamepita na si siri tena. Lakini hawa wakulima kwa miaka 50 na zaidi wameendelea kuteseka kwa sababu ya riba kubwa inayotozwa mikopo waliochukua hapo zamani. Hii si haki kabisa. Bw. Spika wa Muda, labda Sen. Liza anafaa kuja na Mswada katika Seneti hii ili tusizungumze mambo hapa na ilhali Serikali inasikiliza kwa sikio moja na yanapitia sikio lingine. Tunafaa kupitisha sheria ya kusema kwamba mikopo yote ya wakulima inafaa kutozwa riba isiyozidi asilimia tatu au hata chini zaidi. Tukifanya hivyo, wakulima watakuwa na uwezo wa kutoa mazao na kuhakikisha kwamba wamelisha nchi nzima. Watu wakiwa na chakula cha kutosha watakuwa na nguvu na ujasiri mwingi wa kuleta maendeleo katika maeneo yao. Jambo la kuumiza sana ni kuwa sisi wenyewe hapa nchini tunawanyanyasa wakulima kwa njia zote. Mashini za kulima zinauzwa kwa bei ya juu. Pia mikopo kwa wakulima ina riba ya juu nayo bei ya mazao inapungua kunapokucha. Baada ya haya yote, Serikali yetu inaagiza chakula kutoka nchi za nje kupitia wale mabwenyenye walioko ndani ya Serikali. Watu hawa wanapata faida kupita kifani. Tunajua haya yote na tuna mifano mingi. Kwa mfano, Serikali inawakubaliwa mabwenyenye kuleta sukari kutoka nchi za nje. Wakulima watashindwa kuuza miwa yao kwa viwanda vya sukari kwa sababu sukari iliyopo haiuzwi. Hii ni kwa sababu mabwenyenye wanatumia nafasi iliyopo ya COMESA kuleta sukari zaidi kutoka nchi za nje na kuuza hapa nchini kwa bei nafuu. Wakati mwingine hata sukari hii inapakiwa katika mifuko ambayo ina majina ya viwanda vyetu kama vile Sony, Mumias na kadhalika. Huu ni uzembe, uwongo, ufidhuli, unafiki na unyonyaji ambao ni lazima tuupige vita hadi mkulima wa miwa afaidike. Ni lazima mkulima atetewe na kupewa mizizi aingie kabisa ndani ili awe na uwezo wa kulisha taifa la Kenya. Bw. Spika wa Muda, naunga mkono Hoja hii."
}