GET /api/v0.1/hansard/entries/404396/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 404396,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/404396/?format=api",
"text_counter": 240,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Chelule",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13126,
"legal_name": "Liza Chelule",
"slug": "liza-chelule"
},
"content": "Thank you, Madam Temporary Speaker. Asante Sana. Natoa shukrani kwa kunipatia nafasi hii ili nichangie Mswada ulioletwa na Sen. Sang. Kabla ya kuchangia, ningependa kumshukuru sana Sen. Sang kwa kuleta Mswada kama huu wa kutaka kuwa na bodi katika kaunti. Jukumu la bodi hizo zitakuwa ni kuunganisha viongozi katika kaunti zetu na kuongea kuhusu maendeleo katika kaunti zetu. Nilipoona bodi hizo, nilifurahi sana kwa sababu bodi hizo zitaanzia kwenye kaunti na zitaenda kwenye kaunti ndogo, hadi kwenye wodi. Mswada huu utawaelimisha viongozi kwenye kaunti. Viongozi watakuja pamoja na kuongea kuhusu maendeleo katika kaunti yao. Watakuwa pia na nafasi ya kuelewa vile mambo yanafaa kufanywa. Kuna watu ambao wana wasi wasi kuhusu bodi hii. Bodi hii itawaunganisha viongozi na kuwaelimisha pamoja na wananchi. Haja yetu kama Maseneta ni kuhakikisha kwamba tumewafanyia wananchi kazi vile tulivyowaahidi tulipokuwa tukiomba kura. Kazi yetu kama Maseneta ni kuwakilisha serikali za kaunti na wananchi na kutetea pesa ili ziende kwa wananchi. Haitakuwa vyema kutetea pesa ziende katika serikali za kaunti bila sisi kuwa na nafasi ya kujua vile pesa hizo zitatumika. Kwa hivyo, nafurahi kujua kwamba tutakaa kama viongozi wa kaunti na kujadiliana pamoja ili tuwe na mipangilio ambayo kila kaunti inahitaji. Pia, tunafaa kujua shida ambazo zinakumba kaunti zetu. Vikao vyetu katika kaunti havitakuwa vya kuitisha uongozi katika kaunti The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate"
}