GET /api/v0.1/hansard/entries/404398/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 404398,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/404398/?format=api",
    "text_counter": 242,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "lakini vitakuwa vya kubadilishana mawaidha kulingana na vile tunavyotaka kuhudumia wananchi. Bi. Spika wa Muda, kiongozi anaweza kuanzisha miradi na hatamu ya uongozi wake ifike kikomo kabla hajakamilisha miradi yake. Itakuwa vibaya sana kama kiongozi ambaye atakuja nyuma yake ataanzisha miradi mingine badala ya kuikamilisha ile iliyokuwa ikiendelea. Tutakapokuwa na vikao katika kaunti, tutahakikisha kwamba miradi yote ambayo ilianzishwa mbeleni imekamilishwa. Kuna miradi ambayo haijakamilishwa kwa muda mrefu. Miradi hii huwachwa hivi mpaka pesa zinakwisha. Kabla hatujapitisha Katiba ambayo tunayoitumia sasa, tulikuwa na kamati ya maendeleo katika kila wilaya. Bodi hii itafanya kazi kwa niaba ya kamati ya wilaya. Kamati hiyo itakuwa ikifanya kazi na kuchunguza ni sehemu gani ina shida. Mimi natoka Kaunti ya Nakuru ambapo kuna shida ya barabara. Bodi hii itakapoanza kufanya kazi itaweza kujua shida ziko katika sehemu zipi. Kuna sehemu ambazo zina shida za barabara na sehemu zingine ambazo zina shida ya maji. Watu wengine wana shida ya hospitali. Ni jukumu letu kufanya kazi hii kwa sababu tulichaguliwa na wananchi. Watu ambao walichaguliwa walikuwa kama sita. Our work isto provide services to the people. Naunga mkono Mswada huu na kumpongeza Sen. Sang. Watu ambao wanaipinga bodi hii kwa kusema kwamba Sang hata hajaoa wanafaa kujua jambo hili halihusiki na bwana au bibi ya mtu. Bwana ya mtu hawezi kuwa mwakilishi wa bodi na pia mtu hawezi kumleta bwana yake kuwa mwakilishi wa bodi. Yeye alijitokeza baada ya kuona kwamba kuna haja ya kuwa na bodi kama hii. Hakufikiria hivi kwa sababu ya umri wake mchanga. Alifikiria hivyo kwa sababu ana akili nzuri sana. Bodi hii pia itakuwa na viwango vitatu. Kutakuwa na moja katika sub county ambapo mwenyekiti atakuwa Mbunge wa sehemu hiyo. Kutakuwa na kitengo kingine katika wodi ambapo mwenyekiti atakuwa ni Member of County Assembly (MCA). Bodi hizi zitawaunganisha watu wote. Watu wote wataelimika kutokea kiwango cha wodi hadi kaunti. Sisi sote tuna changamoto tunapoendeleza maendeleo katika kaunti zetu. Tutakapokuwa tukikutana katika kaunti, hatutakosa kupeana mawaidha kuhusu vile tunaweza kufanya kazi. Kazi yetu ni kuhakikisha tunawajibika katika kuwasaidia wananchi. Mswada huu umenifurahisha na kunielimisha sana. Sote tutakuwa tukisoma katika ukurasa mmoja. Sasa hivi, tukiulizwa kile ambacho kinaendelea katika kaunti zetu, ingawa tuko hapa kuwakilisha kaunti, utashangaa sana kwa sababu hatujui. Wengine wetu hatujui chochote kinachoendelea huko. Mambo yote kuhusu pesa yamekuwa ni ya siri. Hiki ni kikao ambacho kitatusaidia kujua ni pesa ngapi zimetumwa katika kaunti na ni ngapi zimetumika. Pia, tutajua ni pesa ngapi zimepotea na miradi ambayo inafaa kufanywa. Mimi kama Seneta kutoka Nakuru, nitafurahia kwa sababu nitajua shida ambazo zinakumba sehemu tofauti. Bi Spika wa Muda, kuna mambo ambayo huwa yanasahaulika. Haya ni mambo ya kuzaa na huduma za hospitali. Akina mama na watoto wengi wamepoteza maisha yao. Kama hatutakaa pamoja kama viongozi, hakuna mtu atakayeifikiria shida ya mtu mwingine. Lakini tukikaa pamoja kama Maseneta ambao wanawakilisha watu ambao hawajiwezi katika jamii, kwa sababu hakuna mtu aliye kamili hasa, tutaweza kusaidiana. Jambo hili litatukutanisha na kila mmoja atakuwa amewakilishwa katika kaunti. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate"
}