GET /api/v0.1/hansard/entries/404400/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 404400,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/404400/?format=api",
"text_counter": 244,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Bodi hii pia itatuunganisha pamoja kama viongozi na kutuelimisha. Sisi wote tuna majukumu ya kuchunguza jinsi pesa zinavyotumika katika kaunti zetu. Kazi hii haifanyiki katika kiwango cha Serikali kuu. Sisi kama Maseneta tunaangalia Serikali kuu na pia zile za kaunti. Tunawaakilisha watu wa chini kulingana na Katiba. Haitakuwa vyema kama Seneta kuwa sina jibu la kuwaambia wananchi wakitaka kujua kwa nini hawana hospitali ama huduma zingine. Ni lazima nijue ni pesa gani zitakazotolewa kutoka Serikali kuu. Pia, ninafaa kujua ni kiasi gani cha pesa ambazo zimetumika katika miradi mbali mbali. Hatutaki pesa zitumike katika katika miradi ambayo hatujui. Namshukuru Sen. Sang kwa kuleta Mswaada huu. Kuna mambo ya mipangilio ya maendeleo ya kaunti ama strategic plan ambayo hatujaonyeshwa. Hii itakuwa nafasi yetu pia ya kujua mipangilio ya kila kaunti. Tungependa kujua ni miradi ipi inafaa kupewa kipaumbele. Ikiwa watu wanataka hospitali na barabara, hatuwezi kusema tuwekewe stima kwanza. Hatuwezi kusema tutengenezewe barabara ikiwa hatuna stima. Hii itatupa nafasi kama viongozi kuungana pamoja. Tunafaa kujua ni nani anafanya kazi ipi. Tunafaa kuifanya kazi hii tukiwa na umoja. Sina mambo mengi bali kuunga mkono Mswada huu."
}