GET /api/v0.1/hansard/entries/404401/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 404401,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/404401/?format=api",
"text_counter": 245,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Njoroge",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13158,
"legal_name": "Ben Njoroge",
"slug": "ben-njoroge"
},
"content": "Asante, Bi. Spika wa Muda. Yangu ni kuunga mkono Mswada huu ambao tunauita Sang Bill. Mjadala wenyewe unatutambua katika kaunti hata sisi ambao mara nyingi huitwa nominated . Sasa tumepata kazi ya kufanya katika kaunti ambazo tumetoka, sehemu ambayo tulipigia kura. Mara nyingi, tumekuwa tukienda katika kaunti na kujisikia kama watu ambao wanaomba kusikilizwa. Lakini sasa, Mswada huu umetupa kazi katika bodi. Jambo lingine ambalo ningependa kusema ni kwamba imekuwa vigumu sana kuwasaidia watu walemavu katika kaunti kwa sababu hatujakuwa na mikakati bora. Kila eneno likiwa na uwakilishi hapa Seneti na tujadiliane mambo yanayowakumba watu walemavu, basi mambo haya yataangaliwa vizuri. Nimekuwa nikifikiria kile Maseneta ambao walipewa kura wangewaambia wananchi baada ya miaka mitano. Wananchi ambao waliwachagua hawawezi kuelewa kwamba kuna mambo muhimu ambayo yanapitishwa na Seneti ambayo yanawafaidi katika kaunti. Sasa, vile watahusishwa, kazi yao imekuwa rahisi. Sasa wataweza kuwaeleza kazi ambayo wamekuwa wakifanya. Watu waliopiga kura wangedhani kwamba walidanganywa. Sasa hivi, wamejihusisha moja kwa moja. Jambo lingine ambalo ningependa kusema katika Mjadala huu ni kwamba Mswada huu umeletwa katika wakati unaofaa. Seneti hii inatakiwa kuwa ikifanya kazi ya kusaidia kaunti. Juzi, Seneti ilipokuwa ikizunguka kupokea maoni kuhusu Mswada wa Sang, watu walisusia vikao hivyo. Magavana wengi walisusia vikao hivyo na hawakutaka kukutana na Maseneta. Watu waliwasikiliza county executives na kuvisusia vikao vya Maseneta. Jambo hili litakuwa ngumu sana kwao lakini kulingana na maendeleo ambayo yanatakiwa katika kaunti, bila kuhusisha Maseneta, maendeleo hayatapatikana kwa urahisi. Magavana wanacheza mchezo kwa sababu wakipatwa na shida ambayo wanataka tuitatue kama Seneti, wanatukimbilia. Wakati walisikia Maseneta wanataka kushirikiana nao katika miradi, pia wakawa na wasiwasi. Hawataki kutuona. Ni kwa nini Magavana wanaendelea na hio tabia? Tunajua vizuri kwamba wengi wao walisusia vikao kwenye kaunti kwa sababu ya jambo hili. Inafaa ieleweke vizuri kwamba Gavana sio mwandishi The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate"
}