GET /api/v0.1/hansard/entries/404777/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 404777,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/404777/?format=api",
    "text_counter": 145,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Mwaura",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13129,
        "legal_name": "Isaac Maigua Mwaura",
        "slug": "isaac-mwaura"
    },
    "content": "Bw. Naibu Spika wa Muda, nimesimama kupinga Hoja hii kwa sababu Serikali ama chama kilio na wengi ama wachache kina nafasi ya kuleta miswada na ajenda zao Bungeni Jumanne, Jumatano saa nane na pia Alhamisi. Wabunge wengi wana miswada tofauti ambayo wangependa kupendekeza. Kutokana na Katiba mpya, Bunge hili halifai tu kupatiwa ajenda na upande wa Serikali. Tunafaa kuwa na nafasi ya kuweza kuwasilisha matakwa na jumbe kutoka kwa wale ambao tunawaakilisha, na Jumatano asubuhi tunakuwa na mwanya mwafaka. Ninapenda kupinga kwa sababu wakati huu ndio tunapata nafasi ya kuzungumza kwa sababu mara nyingi wakati ule mwingine hatupati nafasi. Utakuta kwamba ni Mkuu wa Wengi na wengineo ambao wanazungumza. Kwa hivyo, ninafikiri muda huu unafaa kutengwa tuweze kujieleza na kuwashawishi Wabunge wenzetu, ndiposa ajenda zetu pia ziwe na nafasi katika Bunge hili. Ninapinga."
}