GET /api/v0.1/hansard/entries/404845/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 404845,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/404845/?format=api",
"text_counter": 213,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Gathogo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 2715,
"legal_name": "Esther Nyambura Gathogo",
"slug": "esther-nyambura-gathogo"
},
"content": "Ahsante, Mhe. Naibu Spika wa Muda, kwa kunipa nafasi hii. Karibu niulize, pia tukiwa watatu sipati nafasi? Ningependa kuunga mkono Hoja hii, lakini ningependa kusema kwamba hakuna kiasi cha pesa kinachoweza kulipa uhai wa mwanadamu ama kumlipa mwanadamu aliyeathiriwa na ajali. Hata hivyo, ni bora kufikiria kwamba tuko na shida na ni lazima tuitatue shida hiyo. Tukiangalia tutaona kwamba watu wengi wanaumia kutokana na kutolipwa fidia wanapopata ajali. Hata hizo hela kidogo wanazostahili kulipwa ndiyo waweze kujisaidia zinapotelea mikononi mwa watu wengine. Ninaamini kwamba mtu anapoumia, inafaa ajijulie hali yeye mwenyewe. Katika maeneo Bunge, watu wanalia sana. Unapata muathiriwa akisema kwamba kesi yake imemaliza miaka 20, na mwingine akisema kwamba kesi yake imemaliza miaka kumi, lakini unapofuatilia unagundua kwamba fedha za fidia za waathiriwa hao zimelipwa na kupotelea kwa mikono ya watu wengine. Kwa hivyo, hili ni jambo muhimu. Ikiwezekana, inafaa waathiriwa walipwe pesa ambazo zitawasaidia katika mambo ambayo watakua wakifanya, ingawaje hawataweza kufurahia fedha hizo. Mtu hufurahia akiwa na afya njema na uhai. Ni jambo la kuhuzunisha sana familia inapozunguka tu kortini ikifuatilia fidia ya mpendwa wao aliyeaga dunia kwenye ajali pasi na mtu yeyote kuwaonyesha njia. Kwa hivyo, hii ni njia nzuri sana itakayowasaidia watu wetu. Kwa hayo machache, ninaunga mkono."
}