GET /api/v0.1/hansard/entries/404876/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 404876,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/404876/?format=api",
    "text_counter": 244,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Mwaura",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13129,
        "legal_name": "Isaac Maigua Mwaura",
        "slug": "isaac-mwaura"
    },
    "content": "Nasimama kuunga mkono Mswada huu kwa sababu watu wengi sana wameathirika kwa ajali za barabarani. Kuna watu wengi sana ambao wamelemaa na maisha yao yakabadilika kwa sababu ya ajali ya barabarani. Kwa hivyo, ni jukumu letu sisi Wabunge, sio tu kutambua ni ulemavu upi ama ni kiungo kipi kimeathirika bali tuangalie kwa undani zaidi vile ambavyo watu ambao wameathirika wanaweza kujumuishwa katika ujenzi wa nchi hii. Wengi wao hawawezi kutekeleza majukumu waliokuwa wakitekeleza kwa sababu ya ulemavu. Kwa kweli wahenga walisema kwamba ajali haina kinga lakini utakuta kwamba mara nyingi ajali hizi zinatendeka kwa sababu madereva wetu wamekosa kuzingatia zile kanuni za barabara."
}