GET /api/v0.1/hansard/entries/404877/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 404877,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/404877/?format=api",
    "text_counter": 245,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Mwaura",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13129,
        "legal_name": "Isaac Maigua Mwaura",
        "slug": "isaac-mwaura"
    },
    "content": "Bi. Naibu Spika wa Muda, ukiangalia mapendekezo ambayo yako katika Mswada huu, ningependa kuangazia kwamba ni muhimu yule mkurugenzi wa matibabu wa uma pia aweze kushirikiana na baraza la kitaifa kuhusu watu walemavu katika kutambua aina zingine za ulemavu ambazo hazijatajwa katika vipengele vya Mswada huu. Hilo ni jambo muhimu kwa sababu hili jopo limekuwa na uzoefu wa kazi wa kuhakikisha kwamba maswala ambao pengine hayaangaziwi, yanaangaziwa. Sio eti tuu kutoka kwa mtazamo wa afya bali pia katika mtazamo wa kijamii na mtazamo wa haki za kibinadamu. Pia tuangazie, kwa mfano vile ambavyo kumesemwa hapo awali, wale vijana ambao watapata ajali waweze kupatiwa marupurupu na ridhaa ambayo itaweza kuwasaidia."
}