GET /api/v0.1/hansard/entries/404879/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 404879,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/404879/?format=api",
    "text_counter": 247,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Mwaura",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13129,
        "legal_name": "Isaac Maigua Mwaura",
        "slug": "isaac-mwaura"
    },
    "content": "Bi. Naibu Spika wa Muda, pia vile mwenzangu alivyosema nafikiri kiwango cha Kshs.3 million ni cha chini sana. Kama umepoteza viungo vya mwili wako, kama huwezi kufanya kazi, kama huwezi kuhudhuria shule, basi nafikiri lazima tuongeze hizi fedha pengine kuwa Kshs5 million ama Kshs.6 million ndiposa uweze kujimudu. Ni vizuri sana katika sheria hii tuweze kuwa na vipengele ambavyo vitawasaidia waathiriwa kufahamu jinsi ya kupata hizi fedha. Kwa kweli, watu wanaweza kupata uamuzi wa korti lakini tunaona kwamba kuna kule kuchelewa. Wakati mwingine utakuta kwamba kuna matapeli. Watu wanachukua hizi hela na wanaziweka katika mabenki ili wapate riba na ilhali walioumia wanazidi kuteseka. Kwa hivyo, kama tunaweza kuwa na uwazi wa njia ambayo mtu anafaa kuifuata ndiposa aweze kupata zile pesa, litakuwa ni jambo bora sana. Pale mwanzo wakati watu wanatia sahihi katika hii mikataba ni vyema kila jambo liwe wazi. Kusiwe na vijisababu vidogo ambavyo vimewekwa katika maandishi madogo ambavyo watu hawewezi kuvielewa. Nafikiri hilo limependekezwa katika Mswada huu; kwamba wanaweza kukwepa ulipaji kutokana na sababu tofauti tofauti."
}