GET /api/v0.1/hansard/entries/405982/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 405982,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/405982/?format=api",
"text_counter": 85,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Wario",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 252,
"legal_name": "Ali Wario",
"slug": "ali-wario"
},
"content": "Ahsante Mheshimiwa Spika kwa ruhusa yako. Ninachukua fursa hii kumpongeza mwenyekiti wa Kamati hii kwa kazi nzuri alioifanya. Kabla sijampa sifa, sheria iliyoko mbele yetu ni mchanganyiko wa mazuri na mabaya. Tutakaposimama pamoja kukosoa yale mabaya yalioko mbele yetu, bila shaka hii itakuja kua sheria nzuri sana. Nasema hivyo kwa nini? Juzi, Mhe. Halima Ware alizungumzia kuhusu mauaji ya mtoto katika sehemu inayopakana na Tsavo West. Maafisa wa KWS walimuua mtoto. Wakati ripoti ilifika nyumbani, watu kuenda kuchukua maiti, walikuta ilikua imechukuliwa na KWS. Sasa swala nzito tunajiuliza ni; watu hawa wanawala watu? Mtoto huyo walimpeleka wapi? Hakuna mama mzazi anaweza kulia akibingirika akisema mtoto wake ameuawa pale bila jambo hili kuwa la kweli. Damu ilionekana pale, lakini maiti haikupatikana. Pengine Mswada huu utaleta uso wa ubinadamu katika uwindaji wa wanyama na kusimamia mbuga za wanyama. Mwenyekiti alipokua akizungumza jana, alizungumzia faida nyingi, ikiwemo faida ya utalii, GDP na faida aina mbali mbali. Ukumbusho wangu kwa Bunge hili ni kuwa tuwe na sheria bora. Faida haipatikani mpaka tutakapotambua haki ya wale wanaoishi karibu na mbuga za wanyama. Kwa nini niseme hivyo? Wema hulipwa na wema. Mtu amekupa ardhi, mifugo wake hawatoki, shamba lake hawezi kulima na KWS wanaua watoto na kuwaficha! Hapa unalipa wema wetu sisi tunaokupa ardhi kwa ubaya. Kule kwetu tuna Mbuga ya Wanyama ya Kora, Mto Tana, Mbuga ya Wanyama ya Tsavo West na Tana River Primate Reserve. Ardhi yote imeenda na KWS. Pengine sheria iliyoko mbele yetu itapitisha kwamba kila kaunti iwe na mbuga ya wanyama moja na national reserve kadhaa ambazo zitasimamiwa na serikali ya kaunti. Usimamizi wa mbuga za wanyama umewekwa chini ya Serikali ya taifa. Ni vizuri tukubaliane, nyingi ya hizi mbuga za wanyama na reserves ziko katika kaunti. Serikali ya taifa ikisimamia, usimamizi mwingine utafanywa na nani? Kuna maswala nyeti ambayo yanastahili kuamuliwa na serikali za kaunti. Hivyo basi, rasilimali hizi zisimamiwe na serikali ya kaunti. Kama tunazungumza juu ya ukame, ni vigumu kwa waziri kutafakari Tana River iko wapi na ina matatizo gani. Lakini serikali ya kaunti inatambua kweli sehemu ya kusini ya Tana River inastahili kupewa ruhusa walishe mifugo katika mbuga ya wanyama."
}