GET /api/v0.1/hansard/entries/405985/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 405985,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/405985/?format=api",
    "text_counter": 88,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Wario",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 252,
        "legal_name": "Ali Wario",
        "slug": "ali-wario"
    },
    "content": "Ili sheria hii ambayo tunaitunga isigongane na Katiba, mamlaka ya kutangaza sehemu kuwa national park ipitishwe na Bunge. Isipopitishwa na Bunge hivi ilivyo, inafaa kubadilishwa na haifai kupita hapa ndani. Ukiangalia sehemu ya hatia na faini, inanichekeza. Naona mkono wa wakoloni ndani ya hii sheria. Nasema hivyo kwa sababu kuna wanyama katika kifungu cha (a) ambao ukiwaua, utatoa faini ya Kshs20 milioni au kufungwa milele gerezani. Lakini wale wanyama wakiuwa wewe, utalipwa Kshs1 milioni au Kshs3 milioni. Baina ya hao wanyama na wanadamu, nani anastahili kulipwa Kshs20 milioni? Nikiua ndovu, nitafainiwa Kshs20 milioni au nifungwe milele gerezani.Ndovu akiua mtu, familia yake italipwa Kshs1 milioni au Kshs3 milioni kuambatana na hali ilivyo. Jee, wanyama ni muhimu kuliko wanadamu? Je, swali hili tukiulizwa na wananchi ambao wanatutegemea sisi kuwatungia sheria, tutawapa jawabu gani? Hapa naona mkono wa wakoloni. Ili tutoe huu mkono wa wakoloni, ni lazima tuseme kuwa ndovu akiua mtu, familia yake ilipwe Kshs20 milioni au ndovu akiuawa, faini iwe Kshs3 milioni ili kuwe na usawa baina ya sheria na utekelezaji."
}