GET /api/v0.1/hansard/entries/405986/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 405986,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/405986/?format=api",
    "text_counter": 89,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Wario",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 252,
        "legal_name": "Ali Wario",
        "slug": "ali-wario"
    },
    "content": "Kifungu cha 89(f), kinasema kuwa ukipatwa ukilisha ndani ya uhifadhi ya wanyama, hata kama ni mbuzi kumi, utafainiwa Kshs200,000. Pengine dhamana ya wanyama wako haifiki Kshs200,000. Sheria hii itaumiza wafugaji. Ukisoma ukurasa wa mwisho, hifadhi za wanyama ambazo zinahesabiwa hapo ziko katika sehemu za wafugaji. Ni lazima tutambue kwamba kuna haki baina ya mifugo na wanyama hao. Nikimalizia, juzi, maafisa wangazi za juu katika KWS, ambao wote wanatoka katika sehemu ya wafugaji, walisimamishwa kazi. Lakini kabla ya muda wao wakufutwa kufika, ofisi yao ilibadilishiwa watu wengine. Hiyo ni dhuluma. Sisi ardhi yetu imechukuliwa na KWS na tunataka nafasi za kazi kwa watoto wetu. Wale ambao wako katika ngazi za juu wahifadhiwe. Kwa hayo machache, tukirekebisha, nitaunga mkono."
}