GET /api/v0.1/hansard/entries/406076/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 406076,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/406076/?format=api",
    "text_counter": 179,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Kombe",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 250,
        "legal_name": "Harrison Garama Kombe",
        "slug": "harrison-kombe"
    },
    "content": "Ahsante, mhe. Naibu Spika wa Muda. Ningependa kuchukua fursa hii kuunga mkono Mswada huu. Kwa hakika, wanyamapori wanaleta faida kubwa katika taifa hili lakini pia inastahili tufahamu kwamba mwanadamu yuko na thamani kubwa zaidi kuliko mnyama. Hata Mwenyezi Mungu alipoumba mbingu na ardhi, alimuamuru mwanadamu aje ardhini kuwatawala wanyama na awe mwenye mamlaka juu yao. Inatupasa pia tuzingatie kwamba binadamu anathamani zaidi kuliko mnyama. Pendekezo kwamba ridhaa kwa mtu ambaye ameuawa na mnyamapori iwe Ksh3 milioni halijatosheleza. Tuchukulie kwamba mtu huyu ndiye anayeitafutia riziki jamii yake. Mtu huyo anapopotea kwa ghafla, ridhaa hiyo ya Ksh3 milioni haiwezi kukidhi mahitaji ya jamii yake kwa muda mrefu, haswa tukizingatia jinsi shilingi inavyopoteza thamani yake siku baada ya nyingine. Kwa hivyo, wakati wa kupendekeza marekebisho utakapowadia, nitajaribu kuleta pendekezo la kuibadilisha hali hiyo na kuongeza ridhaa kwa mtu atakayeuawa na wanyamapori kutoka Ksh3 milioni hadi Ksh10 milioni. Hata ikibidi jamii ya mwendazake wagawane pesa hizo, kila mmoja atakuwa na kiwango cha fedha kitakachomusaidia. Tuchukulie kwamba aliyeuawa ni mwanamume ambaye amejimudu na kuweza kuoa mabibi 10, alafu uwapatie Ksh3 milioni. Ukiwagawanyia fedha hizo mabibi 10 na watoto wao, kila mmoja anapata kiwango ambacho hakistahili kamwe. Ni pesa ambazo anaweza kuzimaliza kwa mwezi mmoja halafu wabaki wakihangaika. Miongoni mwa wanyama walioorodheshwa, kuna wanyama kama vile nyani na tumbili, ambao wameachwa nje licha ya kwamba hao ndio wanyama waharibifu zaidi wa mimea, na haswa mumea wa mahindi. Inafaa wanyama hao pia wajumuishwe kwenye orodha ya wanyama waharibifu. Vile vile, kuna wavuvi ambao huenda kuvua samaki. Wakati mwingine hukumbana na papa na kupambana nao. Wakati mwingine utapata yule mvuvi amekatwa vipande viwili naye hupoteza maisha yake. Wanyama kama papa inafaa waorodheshwe ndiposa atakayepata hasara ya kuuliwa na papa alipwe ridhaa. Kuna samaki mwingine hatari sana tunamwita pweza. Huyu samaki akikupata katika mwamba utabaki pale pale mpaka bahari ijaye tena upya; utakufa maji. Yule pweza pia angeorodheshwa kama mojawapo wa wanyama ambao wakimwathiri binadamu basi alipwe ridhaa. Ridhaa inayolipwa kwa ajili ya mimea kuharibiwa, kiwango chake ki chini sana. Pana haja, wakati wa marekebisho, tulete marekebisho mwafaka. Kwa mfano, mnazi The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}