GET /api/v0.1/hansard/entries/406641/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 406641,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/406641/?format=api",
    "text_counter": 178,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Muthama",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 96,
        "legal_name": "Johnson Nduya Muthama",
        "slug": "johnson-muthama"
    },
    "content": "Nashukuru sana, Bw. Naibu Spika. Nasimama kuunga mkono Hoja hii. Kuna msemo unaosema ya kwamba “Samaki akianza kuoza, huanzia kichwani.” Ikiwa unataka kusimamisha kuoza kuenea katika mwili mzima, basi lazima ukikate kichwa na kukiondoa. Vitengo vyote vya Serikali vina wasimamizi wake. Kwa mfano, kitengo cha Serikali, hasa kitengo cha Ulinzi, kina msimamizi wake. Taifa nzima sasa limeshuhudia mambo yafuatayo ambayo yanahusiana na usalama wa nchi. Kwanza, kutembea barabarani ni shida. Kufanya kazi ni shida na hata kulala ni shida. Ukiona matukio yalioko sasa, kwa mfano, juzi yupo mtu katika Kaunti yangu ya Machakos aliyefanya kazi yake, akatoka kuelekea nyumbani kwake muda wa saa tatu na nusu usiku. Akiwa njiani, alikumbana na majambazi na akauwawa. Maisha yake yakaishia hapo. Jambo la kuhuzunisha ni kuwa hadi leo, bado polisi wanafanya uchunguzi. Bw. Naibu Spika, ukiangalia mambo yaliyofanyika Baragoi na umkumbuke “ofisa” Waiganjo utaona mambo si mazuri. Mtu huyu aliingia katika ndege ya kikoshi cha polisi na kusafiri pamoja na mkuu wa polisi. Walisafiri katika ndege moja. Ni aibu kubwa kwa sababu Serikali haikujua kwamba yeye alikuwa ni mhuni. Ni mkora aliyekuwa na bunduki na The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate"
}