GET /api/v0.1/hansard/entries/406643/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 406643,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/406643/?format=api",
"text_counter": 180,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "aliyetambulika kama ofisa katika kikosi cha polisi. Baada ya miezi miwili, ndio ilijulikana alikuwa ni mhuni ambaye hakustahili kuwa katika kitengo cha polisi. Bw. Naibu Spika, ukiangalia vile mambo yanavyoendelea katika West Pokot, Turkana na hasa hali ilivyo kule Marsabit, inadhihirisha kwamba kuna shida pahali fulani. Sen. Elachi na Sen. Wangari wamesema kuna mtu ambaye amepigwa risasi katika barabara ya Wabera. Kufikia sasa hakuna mtu aliyekamatwa. Ikiwa tuko katika hali hii, Kenya inaelekea wapi kama taifa? Ushuru tunaoulipa unatumiwa kuwaajiri askari, kuwanunulia bunduki na sare zao. Hata hivyo, ni kama kuna shida fulani katika kikoshi cha polisi. Je, Serikali inaona vile mambo yanavyoendelea? Je, Mhe. Rais mwenyewe anashuhudia mambo haya? Na iwapo anayashuhudia mambo haya, amechukua hatua gani kuweza kusimamisha maafa yanayowakumba Wakenya? Bw. Naibu Spika, mahakama zetu zimekuwa za mchezo. Utamuona mtu aliyeshikwa kwa kumnajisi mtoto mdogo wa umri wa miaka sita, saba, au nane, akiachiliwa kwa bondi ya Kshs150,000 ama Ksh200,000. Vile vile, mwizi anayejulikana kwa ufahari wa wizi anashikwa kwa kesi ya wizi na mauaji, lakini baada ya mwezi mmoja unamuona barabarani akitembea. Sisi hatuwezi kuelewa anapitia mlango gani kutoka jela. Kwa hivyo, ni jukumu la Serikali kuhakikisha kuwa inatoa ulinzi kwa Wakenya wote. Bw. Naibu Spika, mfano mzuri hapa ni mimi mwenyewe. Mkuu wa polisi aliwaondoa askari wangu wote. Hivi sasa mimi sina askari wa kunilinda. Nilipigia simu Inspekta-Generali mwenyewe juu ya jambo hili. Yeye aliniambia kuwa hajui amri ya kuwaondoa askari wangu ilitoka wapi. Alinishauri kuwa niendelee kumuomba Mungu anisaidie. Je, mzee wa kawaida wa Marsabit ambaye hawezi kumpigia simu Inspekta-Generali, atafanyeje? Huu ni mchezo mbaya sana na ni lazima usimamishwe mara moja. Serikali hii imeshindwa kutoa ulinzi kwa Wakenya wote. Askari akishindwa na vita, anainua mikono juu na kusema kuwa ameshindwa, halafu anakamatwa na kufunguliwa mashtaka ama anafanyiwa kile anachotakiwa kufanyiwa. Serikali imeshindwa kutoa ulinzi. Mimi juzi nilisema halikuwa jambo la busara kumnyima Mkuu wa Polisi mamlaka ya kuhamisha askari kutoka stesheni moja hadi nyingine. Pia nilisema ni lazima Inspekta-Generali awe na uwezo wa kuwaadhibu maofisa wake. Mambo haya hayawezi kufanywa na mtu mwingine ambaye yuko nje ya kitengo cha polisi. Maofisa wengi wa polisi hawana nidhamu. Wanafanya kazi vile wanavyotaka kufanya. Tunataka Mhe. Rais awahakikishie wananchi wote usalama wao. Ni lazima aongoze kama Mhe. Rais aliyepewa madaraka na Wakenya wote kuongoza nchi hii. Bw. Naibu Spika, sisi wanasiasa tumehatarisha maisha ya watu wetu. Kila mara tunapenda kuwapiganisha watu wetu. Ukiangalia Kaunti ya Moyale utaona ya kwamba kuna mambo mawili. Wizi wa wakora na mauaji ya kikabila. Nataka mambo haya mawili yatofautishwe. Kuna viongozi wanaogonganisha wananchi. Viongozi hawa ni lazima wakamatwe na kuwekwa ndani. Ikiwa tutawaogopa, basi tutakuwa tumeharibu mambo. Hata kama tunataka waendelee kuwa katika mrengo wetu wa kisiasa, basi tujue kwamba tunawaangamiza Wakenya na taifa kwa jumla. Huu msingi tunaouweka si dhabiti kwa utaifa wetu. Ikiwa tutaendelea hivi, basi itakuwa ni mauaji na mateso kwa wananchi wote. Bw. Naibu Spika, kwa hayo machache, naomba kuunga mkono."
}