GET /api/v0.1/hansard/entries/407554/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 407554,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/407554/?format=api",
"text_counter": 153,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Wario",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 252,
"legal_name": "Ali Wario",
"slug": "ali-wario"
},
"content": "Ahsante sana Bw. Naibu Spika wa Muda kwa kunipa fursa hii. Kifungu 94(1) cha Katiba ya nchi yetu kinatoa uwezo na mamlaka ya utunzi wa sheria kwa watu wa Kenya na hili Bunge. Kwa hivyo, yeyote mwenye ndoto ya kubeba taka na kutuletea na sisi tusifungue kuingalia, hiyo ni ndoto iliyopitwa na wakati. Mimi nina wajibu na Bunge lina wajibu. Kifungu 95(2) kinasema kuwa Bunge ni lazima lijadiliane juu ya matatizo yanayowakumba Wakenya na ipitishe na itafute suluhu. Kwanza kabisa, naunga mkono Hoja hii. Pili, pengine ripoti iliyoletwa hapa ina mapendekezo mazuri na mabaya. Bunge itayachukua mapendekezo mazuri na itarekebisha mapendekezo mabaya ili yawe ya manufaa kwa watu wa Kenya. Kuna watu ambao wamedhulumiwa. Ripoti inasema kinaga ubaga kuwa kuna Wakenya ambao wamedhulumiwa. Wale Wakenya wanastahili malipo. Je, malipo hayo yanatosha? Kwa mujibu wa Ripoti hii, kama hatutaifungua na kuirekebisha, pengine malipo yanayopendekezwa ni madogo kuliko dhuluma waliofanyiwa Wakenya. Ni lazima Bunge liangalie mapendekezo hayo na fidia watakayolipwa wale waliodhulumiwa ili kuona ikiwa inatosha. Ni juu yetu sisi Wabunge kuangalia na kukubaliana. Kama kuna msamaha, ni mikakati gani ambayo tumeweka na ni mchakato gani ambao tumetayarisha ili wale waliodhulumiwa kwa roho safi waweze kusamehe? Siyo tu kupendekeza msamaha, kusema kuwa Wakenya wemekubaliana, Ripoti imepita na maneno yameisha. Ni lazima Bunge liangalie jambo hilo. Nikimalizia, rafiki yangu na Mwenyekiti wa Wabunge Wafugaji, Mhe. Gen. Nkaissery amesema kuwa ametajwa. Wale ambao wametajwa ni haki yao kupewa fursa ili kujulikane kama ni kweli wamehusika ama wametajwa tu. Tume yenyewe ya Ukweli, Haki na Maridhiano ilikuwa na matatizo mengi; mara mwenyekiti achunguzwe, mara The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}