GET /api/v0.1/hansard/entries/411381/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 411381,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/411381/?format=api",
    "text_counter": 41,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Onyonka",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 128,
        "legal_name": "Richard Momoima Onyonka",
        "slug": "richard-onyonka"
    },
    "content": "lazima pawepo mazungumzo ambapo tutakubaliana kuwa kuna mambo makubwa ya kikatiba ambayo yanamkera kila mwananchi humu nchini. Lazima tufanye kazi pamoja. Ingawa kwa upande mwingine mko wengi, tungependa wakati mwingine, kama jana, mtusaidie kupitisha sheria ambazo zitawasaidia wananchi. Kwa upande wetu tungependa kusikia mnayosema ili tuwasaidie kuendeleza Serikali na mshikilie uongozi jinsi mnavyofanya. Hatuna tashwishi kabisa kuwa ninyi ndiyo mlichukuwa kura na kuwa ninyi ndiyo chama kinachotawala na pia mna miaka minne mbele yenu na sharti mtekeleze hili jambo. Lakini lazima pia sisi mtuheshimu kutoka upande huo. Utaniwia radhi ndugu Spika, nikisema kwamba, wewe kama mwenyekiti wa Bunge hili ningependa kukusihi wewe kama rafiki yangu – tumefanya siasa na wewe hapo mbeleni na tukasoma nawe – uwe mtu ambaye ana roho safi ili uwe unatuangalia. Hata kama utaona tunafanya makosa ndani ya Bunge hili uwe unatuongoza na kutueleza mahali ambapo makosa yamefanyika ili tujirekebishe na tuwe na mijadala ambayo itaheshimika Kenya hii. Ahsante, ndugu Spika."
}