GET /api/v0.1/hansard/entries/411772/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 411772,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/411772/?format=api",
    "text_counter": 432,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Ms.) Ibren",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 834,
        "legal_name": "Nasra Ibrahim Ibren",
        "slug": "nasra-ibrahim-ibren"
    },
    "content": "Ikiwa kila kiongozi atazungumza na watu wake, itakuwa vizuri. Lakini unapata kwamba huyu anajaribu kuchochea na yule anatia chumvi upande ule mwingine. Wale viongozi wanalala vizuri kwao nyumbani. Watoto wao wanaenda shule vizuri. Lakini wananchi wale waliowachagua hawana amani. Watoto wao hawaendi shule. Kule shule kadhaa zimechomwa. Shule ni kabila gani? Watoto wote wanasoma katika shule hizo, wawe Waborana, Waburji, Gari, Gabra na Rendile. Kila mtu anasoma katika shule hizo. Shule kama hiyo inachomwa. Ni shule ambayo ina maendeleo zaidi na hufanya vizuri sana katika mitihani ya kitaifa."
}