HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 416417,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/416417/?format=api",
"text_counter": 340,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Bedzimba",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 1933,
"legal_name": "Rashid Juma Bedzimba",
"slug": "rashid-juma-bedzimba"
},
"content": "Ahsante sana Mhe. Naibu Spika wa Muda. Nasimama kuunga mkono Mswada huu kwa sababu haya mazungumzo tunayoyazungumza hapa, tunayazungumza kwa sababu wa usalama wa kitaifa. Usalama wa kitaifa ni jambo la muhimu sana. Na ule ukosefu wa usalama unaonekana taifa nzima, ni kwa sababu hakuna sehemu maalum ya kutoa amri. Ikiwa tutaweza kutoa nguvu ama tutapeleka nguvu kwa ofisi moja, itakua ni rahisi kwetu sisi,kuweza kuelekeza kidole kwa ofisi moja na kuwaambia: “Wewe ndio umekosea. Tueleze ni kwa nini usalama unazorota.” Lakini hivi sasa, imekua ni vigumu kwa sababu, ofisi ya Inspekta- Generali haina nguvu zile ambazo inatakikana kuwa nazo. Mimi nazungumza nikiwa na ujuzi kwa sababu nimefanya kazi katika Kikosi cha Polisi. Kwa hivyo, mimi najua. Ikiwa ofisa wa ngazi ya chini hatajua ofisi ya idara yao kuu ikiwa haina uwezo wa kumuhamisha mahali alipo, kumpandisha cheo ama kumshukisha cheo, basi kazi yake itakua, si ya ukakamavu. Atakua anafanya kulingana na matakwa yake yeye. Lakini akijua kwamba Ofisi ya Inspekta-Generali ina nguvu, inaweza kumtransfer, inaweza kumfuta, inaweza kumuondoa, basi nina imani kwamba atafanya kazi nzuri. Ni kweli kwamba kuna maofisa ambao hawafanyi kazi vizuri. Ni kweli si wengi lakini wachache wapo. Lakini ikiwa tutatoa nguvu kwa ofisi ya Inspekta – Generali, atakua yeye na nguvu za kuweza kumuadhibu. Lakini kwa sasa, naona hata akiseme: “Wewe nakupa uhamisho”, imefikia wakati mtu anaenda kortini kuzuia uhamisho huo. Mimi naomba kwamba tuangalie sana usalama wa kitaifa. Ikiwa twapinga, tupinge kwa sababu. Lakini hivi sasa, hali inavyokwenda, ikiwa tutamnyima nguvu Inspekta –Generali, tutarajie mabaya zaidi yanayoendelea. Kuhusu upande wa Masjid Musa, naona imezungumzwa hapa. Ikiwa mtu hana ufahamu wa mambo yaliotokea, si vizuri kuyachangia ama kuyajadili. Kuna ripoti ambayo tunaitengeneza rasmi, ambayo tutaileta, ambayo pia ni katika usalama wa taifa. Kama ingekua nguvu ziko kwa Inspekta-Generali, leo tungekua twazungumza na Inspekta-Generali na kumuuliza maswali. Hata kama kungekuwa na kidole cha lawama ama cha kupongeza, ingekuwa ni ni kwake, Lakini sasa hatujui ni nani tumlaumu. Katika msikiti huo, kulikua na vikundi vitatu. Kulikua na kikundi kilichokwenda kula chakula. Kuna kikundi kilichokwenda pale kufanya ibada. Kuna kikundi kilichokwenda kufanya ibada na kufanya mengine yao. Kwa hivyo, sio wote waliokuwa katika msikiti ule walikua ni wahalifu. Na ndio maana hivi sasa korti imewaachilia watu zaidi ya 40 wakiwa hawana hatia. Kwa hivyo, mtu asielekeze kwamba Muskiti wa Masjid Musa ni mahali pa uhalifu. Pengine ni watu wachache wanaokwenda kuabudu pale ni wahalifu. Lakini siyo Muskiti wenyewe. Pale ni nyumba ya Mungu. Tunapaheshimu, na kila mtu anapaswa kupaheshimu. Mhe. Spika, ningependa tumpe nguvu I-GP kwa sababu kuna mvutano kati ya makamanda kwenye kaunti. Kamanda mmoja akitoa amri, mwingine anapinga. Kamanda mmoja akiwaamuru askari waende mahali fulani, kamanda mwingini anawaamuru waende mahali pengine. Kamanda mmoja anasema jambo fulani lisifanyike, huku mwingine anasema lifanyike. Kwa hivyo, usalama wa kitaifa utazorota zaidi ikiwa hatutampa nguvu I-GP. Kwa hayo machache, naunga mkono Mswada huu. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}