GET /api/v0.1/hansard/entries/416573/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 416573,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/416573/?format=api",
"text_counter": 149,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Njoroge",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13158,
"legal_name": "Ben Njoroge",
"slug": "ben-njoroge"
},
"content": "Thank you, Mr. Speaker, Sir. Nitazungumza kwa Lugha ya Kiswahili ili wale ambao hawako karibu nasi na wanafuatilia Hoja hii waweze kuelewa vizuri. Ninaunga mkono Hoja ambayo iko mbele ya Seneti siku ya leo. Pia ninaunga mkono majina yote ambayo yameletwa hapa. Hawa ni watu wenye uwezo na maarifa mengi. Ingawa akina mama na vijana wameshirikishwa katika kamati hii, ningependa pia walemavu katika Seneti hii wapewe nafasi ya kutoa mchango wao. Hata hivyo, ninaunga mkono wanachama wa kamati hii ambao wamependekezwa. Nimependekeza walemavu wahushishwe katika kamati kama hii siku zijaazo ili walemavu wengine ambao wako nje ya Kenya wajue ya kwamba Sen. Godliver, Leshore na mimi tunawakilisha vilivyo katika Seneti hii. Sisi tuna uwezo wa kufanya hivyo. Bw. Spika, kwa hayo machache, ninaunga mkono."
}