GET /api/v0.1/hansard/entries/416667/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 416667,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/416667/?format=api",
"text_counter": 51,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Lay",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 1022,
"legal_name": "Joyce Wanjalah Lay",
"slug": "joyce-wanjalah-lay"
},
"content": "Asante sana Bi. Naibu Spika kwa kunipatia fursa hii. Vile vile, ningependa kumpongeza mhe. Sakaja kwa kuleta Mswada huu hapa Bungeni. Kwanza, ningependa kumshukuru Mhe. Rais Uhuru Kenyatta kwa sababu wakati alipotoa hii asilimia thelathini ya utaratibu wa kupewa zabuni alisema ya kwamba hii nafasi ipewe vijana, wamama na walemavu. Hii inamaanisha ya kwamba Rais anaitakia heri nchi hii na pia vile vile anawatakia heri wanawake, vijana na watu ambao wanaishi na ulemavu. Kwa hivyo, ninashukuru sana kwa sababu mhe. Sakaja amekubali kwamba tulete mabadiliko ya kuhakikisha ya kwamba wamama pia wamewekwa katika hii nafasi. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}