GET /api/v0.1/hansard/entries/416668/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 416668,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/416668/?format=api",
"text_counter": 52,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Lay",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 1022,
"legal_name": "Joyce Wanjalah Lay",
"slug": "joyce-wanjalah-lay"
},
"content": "Ukiangalia katika Kifungu 27(1), kinasema kuwa kila Mkenya ako na haki ya usawa. Ako na haki ya kulindwa na pia ya kupata manufaa katika nchi yetu ya Kenya. Kwa hivyo, jambo kama hili litaleta manufaa hasa kwa vijana wetu ambao hawana kazi na ambao wanajiingiza katika mambo ambayo yanahatarisha maisha ya Wakenya wenzao. Pia, wanaingia katika mambo ya mihadarati. Kwa hivyo, nafasi hii ya utaratibu wa kupewa zabuni italeta nafuu katika maisha yao. Vile vile, nikiwa mmoja wao ambao wanatia mkazo katika mambo ya elimu, kunao wengi ambao ninawasomesha kupitia kwa hizo fedha. Ni vizuri watoto hawa wakimaliza kusoma wawe na nafasi katika Serikali yetu. Tukisema ni kazi, nafasi za kazi hazipatikani. Kwa hivyo, ni vizuri waingie katika biashara ili pia wao wawe na fursa ya kujenga nchi yetu."
}