GET /api/v0.1/hansard/entries/416746/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 416746,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/416746/?format=api",
"text_counter": 130,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Chidzuga",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 751,
"legal_name": "Zainab Kalekye Chidzuga",
"slug": "zainab-kalekye-chidzuga"
},
"content": "Asante sana, Naibu Spika. Ninasimama kuunga mkono mjadala huu, na kumpongeza mhe. Sakaja. Ni matakwa ya Wakenya na sisi viongozi kuona kwamba vijana wetu na akina mama wamepata uwezo wa kujiendeleza kimaisha. Lakini, nikiunga mkono Mswada huu, kuna vikwazo ambavyo ni lazima tuvitilie maanani. Kwanza ni kuhusu kusajili kampuni ambako kunahitajika pesa nyingi sana. Tukiangalia, vijana na akina mama hawajaanza kufanya kazi, hizo pesa watatoa wapi? Naibu Spika, tumejitolea sisi viongozi tuwafanyie usajilishaji wa kampuni vijana na akina mama, lakini bado kuna vikwazo vingine. Kwa mfano, kwenye shirika letu la ujenzi; National Construction Authority, ukiaangalia kuna vikwazo vingi. Kuna malipo ya Kshs10,000 ambayo inatozwa. Je, hawa vijana ikiwa hawajafanya hata kazi hiyo, watatoa pesa wapi? Kwa hivyo, ninapendekeza kwamba yale mashirika yanayohusika ya Serikali, yafikirie kwanza kuyaondoa hayo malipo kwa miaka miwili ili hawa vijana na akina mama wajisajilishe. Baada ya miaka miwili, wataweza kulipa kwa sababu watakuwa na pesa. Kama si hivyo, vijana na akina mama hawatazipata hizi kazi hata kidogo. Mhe. Naibu Spika, kuna kile kiwango kingine ambacho ni cha fomu ya CR12. Nacho pia kinahitaji malipo ya juu. Pia tunapendekeza malipo hayo yaondolewe kwa miaka miwili. Baadaye wataweza kuanza kulipia sababu bila kufanya hivyo, hizi kazi zote hawatazipata. Wanahitajika wawe na vyeti lakini hawana kwa sababu hawawezi kuvilipia. Kwa hayo machache, ninaunga mkono Mswada huu. Asante sana."
}