GET /api/v0.1/hansard/entries/417011/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 417011,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/417011/?format=api",
"text_counter": 108,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Dr.) Shaban",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 139,
"legal_name": "Naomi Namsi Shaban",
"slug": "naomi-shaban"
},
"content": "Ahsante sana Bwana Spika kwa kunipa fursa hii ya kuongea juu ya suala hili la Hazina ya Uwezo. Ni kweli kwamba Wakenya wamengojea kwa muda mrefu. Nasimama kumuunga mkono kiongozi ya walio wengi hamu Bungeni. Wakati umefika; chelewa chelewa utakuta mtoto si wako. Bwana Spika, tumengoja kwa muda mrefu sana. Wakati tumengojea hivi kuna umuhimu tukubali kwamba Kenya imebadilika na katika Bunge hili hatuko peke yetu bali tuna wenzetu. Yale ambayo wametaka tubadilishe ni machache tu. Mimi nimeyapendelea hayo mabadiliko kwa sababu kuna umuhimu Serikali kuu ihusishwe wakati tunafanya hizi kazi. Nimependa pale walipotaja kuwa mwenye kusimamia masuala ya maendeleo ambaye ni mfanyikazi wa Serikali kuu na Msimamizi wa Pesa ambaye pia ni mfanyikazi wa Serikali kuu wataweza kuileza Serikali kuu yale yanayoendelea. Kina mama, vijana na wazee ambao wamejiunga kwenye vikundi hivyo wataweza kufanya kazi kutumia pesa hizi taslimu Ksh6 bilioni ambazo zinatakikana kutumika humu nchini ili kuleta maendelea. Muda unakwenda na kwa vile mwaka uko karibu kuisha, naomba wenzangu wamuunge mkono kiongozi wa walio wengi humu Bungeni ili The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}