GET /api/v0.1/hansard/entries/417029/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 417029,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/417029/?format=api",
"text_counter": 126,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Mungaro",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 76,
"legal_name": "Gideon Mung'aro Maitha",
"slug": "gideon-maitha"
},
"content": "Kitu kingine ambacho ningependa kuchangia pia katika Hoja hii ni kwamba pesa nyingi zisitumiwe katika mafunzo. Ninajua ni desturi ya Wizara nyingi kuwa wakipata kiwango fulani kinaweza kutumika katika mafunzo, wao hutumia kiasi kikubwa kushinda kile ambacho kitawafikia vijana na akina mama mashinani. Kwa hivyo, tunaomba watumie pesa kidogo kwa mafunzo na nyingi zienda mashinani. Vile vile, ningependa pia kuwauliza wenzangu tujaribu hasa kuchagua vijana na akina mama katika kamati hii ili isije ikawa pesa ni za akina mama na vijana lakini kamati ni ya wazee."
}