GET /api/v0.1/hansard/entries/418022/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 418022,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/418022/?format=api",
"text_counter": 275,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Bw. Spika wa Muda, watu ambao tunazungumzia hapa tunawaita wazee. Lugha ambayo inatoka hapa ni kwamba ni watu ambao yafaa wasaidiwe. Kwa hali ya haki na mbele ya Mwenyezi Mungu, hao sio watu wanataka misaada bali haki yao. Shirika linalokusanya hela na kuweka kwa niaba ya watu wanaozeeka limedhibitisha kwamba pesa ambazo zimekusanywa hadi leo zikitumiwa vyema zinaweza kuwafanya watu hawa waishi maisha yanayofaa. Kulingana na yale ambayo yamesemwa na wenzangu hapo mbeleni ni kwamba kama kuna shirika ambalo lina fedha za kujimudu ni lile la uzeeni. Shirika la NSSF leo limebadilisha kazi ambayo linastahili kufanya na imekuwa ni kama ng’ombe wa kukamua maziwa na kuwanyima wanaostahili na kuwapa wale ambao hawastahili. Ukiangalia hivi leo ni dhahiri kwamba pesa ambazo zimewekwa, kiasi kikubwa kimeingia katika mifuko ya walafi ambao hawana huruma kabisa kwa wanaotozwa ushuru. Bw. Spika wa Muda, mchango unaotolewa na wafanyakazi maskini ambao ni wa hali ya chini kabisa ndio pesa ambazo tunapeleka NSSF. Sasa hivi pesa hizo zimekuwa ni za wale wanaokaa juu na wale ambao wanakaa chini hawapati. Nitakuchukua kama shahidi kwamba katika kaunti unayotoka umepokea malalamishi na manung’uniko ya watu wakisema kwamba tangu wastaafu, ambayo ni miaka ishirini, mtu hawajapata malipo yao ya uzeeni. Serikali haistahili kugusa hela ya watu. Shirika hili likiwacha kufanya biashara ya wizi ambapo wanatafuta sehemu moja ya ploti ya Kshs4o milioni lakini mwishowe inagharimu Kshs400 milioni. Kwa hivyo, takriban Kshs360 millioni inaingia kwa mifuko ya wezi. Itasaidia sana kuona kwamba yule maskini ambaye anastahili anafaidika. Namshukuru Sen. (Prof) Lesan kwa kuleta Hoja hii. Kwa sasa tutazungumza na kufanya taifa lote kuelewa kwamba tunafahamu kuna wezi ambao wanaiba na kunyang’anya maskini. Sen. G. G. Kariuki amesema kuwa idadi ya watu ambao ni wazee na wanahitaji msaada ni 1.2 milioni . Hii inamaanisha kwamba hii ni asilimia 3 tu ya wananchi wa Kenya. Lakini sio hawa tu ambao wanahitaji kusaidiwa. Kati ya wale millioni moja na laki mbili, labda ni mia saba au mia nane ambao watahitaji kusaidiwa. Mimi nataka kuzungumza kwa Serikali. Sisi tunasema hapa tunaelewa lugha ya pesa. Sisi sio watu ambao tunazungumzia maneno ya pesa na hatuelewi. Tunajua kwamba ukichukua watu 800,000 na kila mmoja apewe Kshs.2,000, hiyo ni Kshs1.6 bilioni. Hii ni kidogo sana. Kwa hivyo, Serikali haiwezi kutumia lugha ya udanganyifu kuwadanganya wananchi ambao inastahili kuwasaidia, kuwaelimisha, kulinda na kukinga maisha yao ili waache kudanganya kwamba tumetoa Kshs2,000 kwa maskini ambao wanaishi pale vijijini ni kama wao sio wananchi. Tukifanya hivyo, tutajiletea balaa katika nchi hii na tutaendelea na kukumbana na laana katika taifa letu. Njaa haitaisha kwa sababu tunachukua mahali ambapo hatukupanda. Tunavuna, kula na kushiba ilhali anayestahili akiwa anaumia. Bw. Spika wa Muda ningependa kusema kwamba Serikali ingetoa pesa, singesimama hapa kuuliza Sen. (Eng.) Karue ni nini anamaanisha na mambo ya kitambulisho cha kitaifa ingelikuwa tunaongea lugha moja ya kusema Kshs5,000 ama Kshs10,000 ipewe wale watu waishi maisha ambayo wanastahili katika nchi yao. Uchumi wa nchi unaongozwa na mabebari ambao baba zao walifanya hayo, watoto wao wanafanya hayo na wajukuu pia wanangoja kuja kufanya mambo hayo. Taifa The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}