GET /api/v0.1/hansard/entries/418024/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 418024,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/418024/?format=api",
"text_counter": 277,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "hili linaelekea katika ulingo wa hatari ambao haujawahi kuonekana. Kwa sababu sisi tunafikiri kwamba tukinunua bunduki tuweke katika store yetu, ile kununua magari ya polisi tunaweza kunyamazisha wananchi kudai haki zao. Ningependa kusema kwamba huu ni moto tunawasha na siku zijazo itakuwa ngumu sana mtoto wa tajiri kuanzia tosti ya kwanza hadi ya mwisho kwa sababu kutakuwa hakuna nafasi. Kila mtu atakuwa mbioni. Serikali hii na ile inayokuja, na ninawaambia wenzangu hapa, watatoka na bunduki na wananchi hawataogopa kupambana nao. Risasi zitapigwa na mwananchi hatasikia. Risasi zitatupwa na watu watapigwa lakini maskini atasimama na umaskini wake na kusema kwamba anatetea haki yake. Masikini ataendelea kuishi na umaskini wake na kutetea haki zao. Ikiwa kuna haki ambazo hazipatikani, atasimama na kuzitetea. Watoto wetu ambao wamesoma lakini wamekosa kazi ni wengi sana. Hata hivyo, kuna Kshs430,000,000 zinazopotea katika njia ambazo hazijulikani na bado tunasema taifa hili halina pesa. Kati ya pesa hizo, Kshs180,000,000 zinatumika kulipa marupurupu. Marupurupu hayo hayalipwi mwendeshaji wa mikokoteni ama mlinda ng’ombe ambaye umemwacha katika kaunti. Marupurupu hayo yanalipwa kuwaongezea walio na pesa. Kazi yetu imekuwa kutumia pesa kununua maua ya kuzika masikini ambao wanatafuta kura na nafasi za kuongoza. Tumekuwa tukisema tunataka watu waache kula rushwa. Tunazuia rushwa lakini magendo inafanywa kila siku. Mimi ni Mkristo. Kuna Kitabu ambacho huniambia kwamba kuna punda aliyekataa kwenda akiwa amebeba tajiri wake. Punda huyu aliongea kama mtu na kusema; “Usinipige. Nimechoka kwani siku zote nimekubeba. Sijawahi kusita kukubeba. Kwa nini unanipiga?” Mwananchi wa Kenya yuko karibu kuongea kama punda. Kama hatutabadilisha mambo, tutakuwa na kilio na kusaga meno."
}