GET /api/v0.1/hansard/entries/418031/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 418031,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/418031/?format=api",
"text_counter": 284,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Nimeshukuru sana kwamba hatutawaondoa wazee katika nyumba zao. Tuna shida kubwa Kilifi. Sio kila mtu ambaye anafaa kupewa msaada huu wa Kshs2,000 huupata. Lazima tuchunguze na kujua ni kitu gani ambacho kimekosa kwa sababu sio kila mtu anayepata Kshs2,000. Tunatoa shukrani kubwa kwa Serikali yetu ya Jubilee. Ni wangapi wetu ambao wanaweza kupeana Kshs2,000 kwa wazazi? Siulizi kuhusu watu walio na kazi kubwa kama sisi. Nauliza kuhusu mwananchi wa kawaida. Ni wangapi ambao wanapeana Kshs2,000 kwa baba ama mama? Huu sio msaada haba. Watu wa Kilifi wanahitaji title deeds na sio pesa tu. Ukitazama runinga, utaona kwamba watu wa Kilifi wamekuwa wakiwauwa watu wazima ambao wanakula chakula ambacho kingekuwa kikiliwa na watoto wetu. Pia, kuna wazee ambao wamekatalia titledeeds . Inabidi watu wa pale mtaani ili waipate ile title deeds . Twaomba Serikali yetu ya Jubilee itupe title deeds . Twaiomba iwasaidie wazee. Inafaa wazee wapate matibabu na walipe pesa kidogo kwa National Hospital Insurance Fund (NHIF) na kuzeeka wakijua wana dawa na misaada mingine midogo. Kwa niaba ya watu wa Kilifi; naomba Serikali itusaidie. Naomba title deeds zitolewe na kila mzazi apewe kiwango cha msaada ambacho Mkenya mwingine wa miaka 70 atapewa. Mara nyingi, huko Kilifi, wamama hawapewi pesa hizi. Wanaume ndio wanaopewa kwa sababu wao ndio wenye boma. Mtu mzee si lazima awe mwanaume. Kule tunanyanyaswa kama akina mama kwa jinsia. Wale nyanya wote hawako katika orodha ya kupewa makadirio ambayo yamependekezwa na Serikali. Naunga mkono Hoja hii. Asante."
}