GET /api/v0.1/hansard/entries/418205/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 418205,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/418205/?format=api",
"text_counter": 110,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Boy Juma Boy",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 758,
"legal_name": "Boy Juma Boy",
"slug": "boy-juma-boy"
},
"content": "Asante sana, Bw. Spika wa Muda. Kama Mkenya mimi ninasema kwamba hii ni ripoti nzuri, lakini kama mtu wa kutoka pwani, haifai. Imeeleza vile Bandari ya Mombasa ni nzuri, lakini haikueleza maneno kama mtu wa pwani. Ripoti hii haituambii ni vijana wetu wangapi kutoka pwani ambao wameajiriwa kazi Kilindini. Ripoti hii inatueleza vile Bandari ya Mombasa inafaa Kenya nzima wala si pwani. Shida tunayoipata sisi kule pwani ni kwamba, tunatumika kama ngazi. Ukweli ni kwamba bandari hii iko pwani na haina haja ya kuelezwa na kuna nyingine kule Kisumu. Sasa utaona ya kwamba sisi kama watu wa kutoka pwani hatunufaiki. Idadi ya vijana wanaotoka pwani ambao wameandikwa kazi pwani kulingana na takwimu ni wachache muno. Huo ndio ukweli wa maneno na ndio maana tunasema kwamba Kenya ni nchi moja lakini kuna mambo mengine ambayo ni lazima yabadilike. Haifai watu wengine kubaguliwa wakati wengine wanapokula. Kulingana na takwimu zilioko wale ambao wamechukua nafasi za management katika hiyo bandari wanatoka wapi? Sina haja ya kusema."
}