GET /api/v0.1/hansard/entries/418209/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 418209,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/418209/?format=api",
"text_counter": 114,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "rasilmali ya nchi hii. Itafaa zaidi ikiwa watu wa pwani watafaidika sana kutokana na bandari hii. Lakini sisi tukizungumza ni kama waombaji wa mali na ilhali sisi ni wazalishaji wa mali katika taifa hili. Bw. Spika wa Muda, watu wa pwani tunajulikana au kusifika sana mara mbili kwa mwaka. Mara ya kwanza ni wakati wa maonyesho ya kilimo ya mkoa wa pwani. Tunajulikana sana wakati wa sikuu za Krismasi mwezi wa Desemba. Kuna baadhi ya wageni ambao huzuru maeneo ya pwani wakati wa Pasaka. Kwa hivyo, nikiwa kama Mkenya ninasema kwamba hii ripoti ni nzuri lakini kama mtu wa pwani, hakuna jambo lolote la kujivunia kuwa Mpwani na kuwa na nguvu na ari ya kusherehekea. Pengine msemo maarufu kuwa “Pwani si Kenya” unapata mizizi kwa sababu ya mambo haya. Vijana wa “digital generation” au kisasi cha kisasa wanajua haki zao. Kwa hivyo, ikiwa hawa vijana hawataona haki yao, basi itakuwa ni mtihani. Ukweli ndio huo, hata kama ni uchungu. Bw. Spika wa Muda, swala la bypass ya Dongo Kundu limekuwa likizungumziwa miaka nenda miaka rudi. Jambo hili limekuwako hata kabla ya mradi wa Bandari ya Lamu kuzinduliwa. Barabara hii inaweza kuwasaidia watu wetu kuvuka upande wa pili wa Kwale na si lazima watumie feri. Miaka nenda, miaka rudi, tumesikia kuwa barabara hii itajengwa. Pengine ulegevu ni kwa sababu barabara hii itawafaidi watu wa pwani. Lakini ikifika wakati wa kuomba kura, jambo hili hupewa uzito sana na wanasiasa. Wanasiasa hawa huwahidi watu wa pwani maendeleo kochokocho ikiwa watachaguliwa. Wao husema barabara hii itajengwa ikiwa watapata kura zetu. Lakini maneno haya matamu huisha na kampeini. Baada ya uchaguzi, inakuwa ni ahadi baada ya ahadi. Miaka nenda, miaka rudi, hali haibadiliki. Ni kama hadithi za alfu lela ulela. Bw. Spika wa Muda, kuna mapato mengi yanayotokana na Bandari ya Mombasa. Mfereji wa kupeleka mafuta katika maeneo mengine ya nchi unaanzia Mombasa. Lakini ni watu wangapi ambao wanafanyakazi katika bandari hii? Hili ni swali ambalo linahitaji majibu. Ni wenyeji wachache sana wanaofanya kazi katika bandari hii. Sitaki kusema sana kuhusu bandari hii. Ukiangalia kampuni ya KPRL ni majonzi matupu. Kampuni hii imeachwa kufa kwa sababu iko pwani. Wakati huu tunazungumza kuhusu ujenzi wa kampuni nyingine kule Isiolo na kwengineko. Lakini hii ya pwani kama ingelikuwa mahali pengine popote nchini, ingeshughulikiwa vilivyo. Lakini kwa sababu iko pwani haishughulikiwi na mtu yeyote. Bw. Spika wa Muda, ninaunga mkono ripoti ingawa kama mpwani sioni maana yake. Ni lazima ukweli usemwe. Kuna “ukenya” na “upwani” kwa sababu Kenya ni yetu sisi sote na pwani ni moja ya sehemu za Kenya. Sisi tunaona si sawa kwa sababu tunaonewa. Hii ni hatari na huu ni ubaguzi mbaya sana. Ningetaka kuwaambia kwamba, hawa akina Sen. Hassan ni dotcom na hawatakubali mambo haya ya kunyanyaswa kila siku. Kwa hivyo, tukitaka kuishi na hawa watu wa Pwani vizuri na kwa amani ni lazima wapate haki yao. Si nyinyi peke yenu kuchukua huku, watu wa pwani wakitazama. Hii si hali halisi. Bw. Spika wa Muda, leo hii kaunti yetu ya Mombasa, iwe pia inapewa pesa kutoka kwa Bandari ya Mombasa hata kama ni asilimia kidogo. Tukisema hivyo, tunaambia kwamba hii ni rasilmali ya kitaifa. Mbona msijenge yenu kule Nakuru ama Kericho? Hatukuomba Mwenyezi Mungu atuweke pwani bali tulijikuta huko. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}