GET /api/v0.1/hansard/entries/419569/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 419569,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/419569/?format=api",
"text_counter": 263,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Muthama",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 96,
"legal_name": "Johnson Nduya Muthama",
"slug": "johnson-muthama"
},
"content": "Asante sana, Bw. Spika wa Muda. Nasimama kuunga mkono Hoja hii. Ningependa kuwashangaza kwamba jana nilifuata kwa karibu sana mambo ya ndege iliyopotea katika nchi ya Malaysia. Kilichonishutua si kupotea kwa hiyo ndege, bali ni kuona habari kwa mtandao iliyotiliwa mkazo kwamba Kenya kupitia watumishi wake wa juu Serikalini imepoteza kiasi cha Kshs4 billioni. Hiyo ndio ilikuwa sifa ya taifa hii. Wakati wale wanalilia ndege, inasemekana kwamba sisi hapa kwetu tunaendelea kupanua wizi kwa njia isiyoaminika. Ilinibidi nijiulize kama kweli tuna taifa ambalo tunaweza kujivunia au tunakaa kwa kuvumilia. Uamuzi wangu ni kwamba tunaishi kwa kuvumilia. Bw. Spika wa Muda, kama taarifa ulimwenguni inasema kwamba tumepoteza Kshs4 bilioni ilhali tuna matatizo ya walimu wakiwemo wale wa vyuo vikuu. Wacha tuseme ukweli. Ni vigumu sana kuwaandama wezi wanaoiba pesa za Serikali katika taifa hili. Hii ni kwa sababu wamebadilisha wizi katika taifa letu. Mhe. Boni Khalwale alikuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Public Accounts Committee (PAC). Vile vile Sen. (Prof.) Anyang’-Nyong’o alikuwa katika Kamati ya Public Investments Committee (PIC). Mimi katika Bunge la Kumi nikiwa Kiranja wa Serikali, nilishangaa kwamba tulikuwa tunachunguza vitabu vya matumizi ya pesa za Serikali vya miaka saba iliyopita. Baadhi ya wale waliohusika na wizi hata walikuwa wamekufa au hawapatikani. Bw. Spika wa Muda, ili tuende mbele, kama Rais anapenda nchi hii na kuhurumia masikini, anafaa kuwaandama wale wanaoiba pesa za Serikali hivi sasa na wala si kesho. Tunafaa kuanza na Magavana wanaoiba pesa hivi sasa. Tunakaa na kusema kuwa tutachukua hatua. Je, baada ya miaka kumi tutasaidia vipi? Mambo ni yale yale kwa Mawaziri. Mambo ya reli na laptops yako vivyo hivyo. Wengine wetu wanajifanya kuwa wanatetea Serikali lakini kesho tutakuja papa hapa kusema mambo ya Serikali tuliotetea. Ukweli ni kwamba ni watoto wa masikini wanaoumia. Watoto wa wale wanaoiba pesa hizo wanasomea ulaya. Watoto wanaosomea hapa nchini na kupata matatizo ni wale wa masikini. Tunarudia maneno aliyosema J.M. Kariuki kwamba hii ni nchi ya billionaires kumi na masikini 40 millioni. Bw. Spika wa Muda, wakati ni sasa na wala si kesho. Bw. Matemu alichaguliwa katika kitengo cha kuandama wezi juzi. Kama hataki kuwashika wanaoshiriki ufisadi, anafaa kuondoka ili tuchague mtu mwingine anayeweza kuwashika watu. Hatuwezi The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}