GET /api/v0.1/hansard/entries/421644/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 421644,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/421644/?format=api",
    "text_counter": 250,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": "Asante sana, Bw. Spika wa Muda. Kwanza, nataka kumtumia heko sana aliyekuwa Mkuu wa Sheria katika nchi yetu ya Kenya, Sen. Wako, kwa Hoja hii. Kwanza, ni kwamba wananchi wa Kenya mpaka hivi sasa tokea tugeuze Serikali yetu iende mashinani, yaani, serikali ya ugatuzi, wengi hawajaelewa maana ya serikali za ugatuzi. Kwa hivyo, kunao umuhimu kwa Serikali kufanya juhudi ya aina yoyote ili watu waelewe uongozi na maana ya ugatuzi katika serikali za mashinani. Mimi nataka kuuliza tu kwamba wananchi wengi wanajua kwamba kuna seneta, gavana, mbunge wa maeneo na vile vile wabunge katika serikali za mashinani. Wananchi wengi hawaelewi tofauti ya mheshimiwa mbunge katika bunge la kitaifa na mheshimiwa katika bunge la mashinani. Kwa hivyo, kunahitajika Hoja kama hii kutiwa maanani zaidi ili kuona ya kwamba wananchi wanaelewa haswa uongozi wa aina hii ya ugatuzi unaweza kueleweka namna gani. Kwa maoni yangu, naona kwamba uongozi huo bado haujafahamika na wananchi. Kuongezea ni kwamba vile vile, sisi ambao tunatoka Kilifi, tuko na chuo kikuu kimoja. Wengine wamebahatika kupata vyuo vikuu vingi lakini sisi tunasema kwamba kunao umuhimu katika silabasi ya wanafunzi wa vyuo vikuu, wanafunzi wa sekondari, wanafunzi wa shule za msingi na silabasi ama somo kuhusu katiba ili watoto wetu wanapokuwa, waelewe Katiba ya nchi yao. La mwisho mimi ningependa kusema kwamba hivi juzi kumekuwa na mtafaruku wa kutangazwa kwamba watu wakatwe mishahara. Jambo hili ni jambo gumu. Hata katika sheria ya wafanyakazi ulimwenguni zinasema ya kwamba mwananchi anayefanya The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}