GET /api/v0.1/hansard/entries/421646/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 421646,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/421646/?format=api",
    "text_counter": 252,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "kazi mshahara unaweza kuwachwa pale ama kuongezwa lakini sio kupunguzwa. Kwa hivyo, itakuwa makosa kwa mtu yeyote katika nchi hii kusema kwamba watu wapunguziwe mishahara. Mimi sikubaliani na kitu kama hicho. Sio mimi tu lakini najua kwamba kuna Waheshimiwa wengi ambo wamechukua mikopo mikubwa ambayo wanalipa. Saa hizi, mishahara wanayopata ni duni. Ukisema akatwe pesa asilimia 20, ataenda nyumbani bila pesa. Hivyo, tutakuwa tumeongeza ufisadi kwa sababu lazima mheshimiwa aendelee kuishi na anapofika katika eneo lake la Bunge, aweze kuonekana kwamba anatoa pesa katika harambee. Ikiwa sheria hii itafuatwa, ya kusema watu wakatwe mishahara kwa kiasi fulani, itakuwa makosa. Kulingana na Katiba, Kipengele 41, kila mwananchi ana haki ya heshima katika kazi yake. Kila mwananchi ama mfanyikazi ana haki ya kupata mshahara ulio sawa. Itakuwa aje mtu mmoja anaposimama na kusema mishahara ikatwe? Hiyo naona si haki."
}