GET /api/v0.1/hansard/entries/421666/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 421666,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/421666/?format=api",
    "text_counter": 272,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "March 11, 2014 SENATE DEBATES 46 Sen. Muthama",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Asante sana, Bw. Spika wa Muda. Nasimama kuunga mkono Hoja hii. Bw. Spika wa Muda, mimi ni mmoja kati ya wale waliofanya kazi ya ziada sana katika Bunge la Kumi kuuza Katiba hii mpya. Malengo na mategemeo yetu yalikuwa kutoa pesa kutoka kwa ofisi ya juu hadi mashinani. Tulitaka kuona kwamba wananchi wanapewa uwezo wa kupanga na kulainisha mambo yao. Ninamshukuru mwenzangu, Mkuu wa Sheria aliyestaafu, kwa kufanya jambo nzuri sana la kuleta Hoja hii na zingine kuhusu elimu na mambo mengine. Hii inaonyesha umaarufu wake. Bw. Spika wa Muda, ni kweli kuwa wananchi wanataka kufunzwa na kuelezwa. Haya yalianza na Mhe. Boni Khalwale aliyesema kwamba mafundisho yapelekwe hata katika shule zetu ili wanafunzi waweze kuelewa maana ya Katiba mpya na serikali za ugatuzi. Tuna viwango vitatu vya uongozi katika taifa letu. Kiwango cha kwanza ni Serikali inayoongozwa na Rais mwenyewe. Cha pili ni Seneti na serikali za kaunti. Katika serikali za kaunti kumekuwa na utata mwingi sana na kutoelewana. Wananchi hawana habari kwamba waliwachagua Wawakilishi wa kaunti kuangalia, kuchunguza na kuandama maspika wasiibe na kufanya mambo mengine. Wamesahau kazi hiyo na kuchaguliwa katika mabaraza ya maspika. Wameungana na maspika na kupanga mambo yao. Mpaka leo, wananchi hawajui ni magari mangapi ambayo serikali hizo zinafaa kuwapa magavana. Wananunua vile wanavyotaka. Wananchi wakiwaona wanafikiri wao ni kama Rais. Wananunua hadi magari 20 ya kuwafuata wanakoenda. Wananchi wakiwaona hawajui hata hayo magari yamepeanwa na nani. Bw. Spika wa Muda, mipango yetu ni kuwa na maji, hospitali, elimu nzuri kwa watoto wetu na barabara. Ukimpatia Mwafrika maendeleo hayo, hataki jambo lingine. Lakini sasa imekuwa ni kazi ya uzembe na kuharibu. Hiyo ndio maana tunataka mambo haya yapelekwe haraka. Kama tunataka kuwafunza Magavana wanaofuja pesa na kuiba, ni lazima sisi wenyewe tujiulize: Je, tunapoongea mambo ya mishahara ni wananchi wangapi Kenya wanapata kitita cha zaidi ya Kshs200,000? Hivi leo, asilimia 50 ya pesa zinazokusanywa katika taifa letu zinatumika kulipa mishahara. Kati ya hii asilimia 50, asilimia 48 inaenda kwa wale walio na vyeo vya juu. Sasa tutapunguza mishahara kumsaidia wa juu ama chini? Kama tunataka kulainisha taifa hili ili tusiwe kama taifa la Ugiriki, ni lazima tuangalie mapato yetu ni kiasi gani. Tusikae hapa na kuona ni pesa ngapi tutachukua, kisha tukose kuona safari ya mwendo mrefu tunayoenda. Itakuwa ni jambo la kuudhi sana kuona kwamba anayepata mshahara wa juu Kenya hapiti Kshs300,000. Ingekuwa vizuri kama mtu wa chini ambaye ni askari anayepata mshahara wa Kshs11, 000 angepata Kshs40,000. Hii ingemaliza wizi. Bila mabepari wenye pesa ambao wanaweza kununua kile wanachotaka, bei ya vitu itaenda chini. Lakini tukiwa na watu kumi ambao wanaweka Kshs5 milioni katika akaunti zao kila mwezi, bei ya vitu haitapungua. Kwa hivyo, sikubaliani na hatua ya Rais ya kukatwa asilimia 20 ya mshahara wake. Tunataka apunguze mshahara wake hadi Kshs300,000. Yeye anapewa magari, askari, stima na kila kitu. Je, huu mshahara wa Kshs1 milioni ni wa nini? Wacha tuongee ukweli kwa sababu ikiwa tutaongea ukweli, tutapeleka taifa hili mbele. Tusipoongea ukweli, tutazunguka tu bila kwenda mahali popote. Bw. Naibu Spika wa Muda, naunga mkono. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}