GET /api/v0.1/hansard/entries/421667/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 421667,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/421667/?format=api",
"text_counter": 273,
"type": "speech",
"speaker_name": "March 11, 2014 SENATE DEBATES 47 Sen. Kisasa",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Bw. Spika wa Muda, naunga mkono mjadala huu wa leo. Tumesema kuwa wanafunzi wanafaa kufunzwa kuhusu Katiba shuleni. Je, wale vikongwe ambao wako nyumbani? Ningependekeza kuwa tukiwa kanisani tunaweza kusoma kipengele kimoja. Kwa mfano, kwenye ajali utakuta watu wamejazwa kwenye matatu moja kama ambao wanabebwa bure. Kwa hivyo, wakielimishwa kuwa matatu ndogo inafaa kuwabeba watu 14 tu, hawatajaa. Hii itapunguza visa vya ajali nchini. Bw. Spika wa Muda, pia Magavana hawajui majukumu yao kwa sababu hawakufundishwa vile Katiba inataka. Utawakuta wakiajiri watu waliowapigia kura tu kwa sababu wanajiona kama wao ndio ndume wanaoweza kufanya vile wanavyotaka, bila kuzingatia Katiba. Hoja hii imechelewa sana. Tungefaa kuenda kwa haya mafunzo kabla hata kuja katika Seneti au kuwa Gavana au kazi nyingine yeyote. Bw. Spika wa Muda, Hoja hii ni ya maana sana na namsifu Bw. Wako kwa kuileta. Naomba sote tuiunge mkono."
}