GET /api/v0.1/hansard/entries/423404/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 423404,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/423404/?format=api",
    "text_counter": 194,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": "Asante sana, Bw. Naibu Spika. Kwanza, nataka kumshukuru sana ndugu yetu, Sen. (Dr.) Boni Khalwale, Seneta wa Kakamega, kwa kuleta Hoja huu na umuhimu wake ili tuweze kuelewa maonevu kama haya. Mimi, kama mtu aliyekuwa Hakimu hapo awali na nikastaafu, ni jambo la kusikitisha hasa tukizingatia maswala ya wale watu waliopigania Uhuru katika nchi hii. Swali letu ni hili: Kwa nini watu walipigana? Tumesema ni kwa sababu ya mashamba. Mashamba ni mojawapo kati ya maonevu ambayo watu wa Pwani na sehemu zingine kama Bonde la Ufa waliyofanyiwa. Mashamba mengi ya watu wa Pwani yalitolewa kama zawadi kwa wale watu ambao walisadia Serikali. Jambo muhimu pia ni kuona ya kwamba maonevu mengine ni kama vile wewe kama unatoka Pwani na unaitwa Suleiman, Omar ama Khamis, wewe ni mtu unayetakikana ulete kitambulisho cha babu yako, nyanya yako, babako na mamako ili upate kitambulisho cha kitaifa. Ikiwa wewe ni Stewart Madzayo, wewe unaambiwa hauna haja ya kuleta vitambulisho za wazazi wako ili upate kitambulisho cha kitaifa. Mambo yanakamilishwa kama kawaida. Haya ni maonevu na huu ni kama ubaguzi mambo leo siku hizi."
}