GET /api/v0.1/hansard/entries/423410/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 423410,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/423410/?format=api",
"text_counter": 200,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Sasa, kumezuka Wazungu weusi ambao walikuwa na njia zao walizokuwa wakitumia; wakienda njia ambazo wengine hawawezi kufika na wakipewa ile signature ya rangi ya kijani; halafu wanakuja huko, wanatengeneza fence na wanawaondoa wale wakaazi wa maeneo kama yale. Tunasema kwamba maonevu kama haya ni mojawapo ya yale tunayosema kwamba wale waliofurushwa kutoka katika mashamba yao pia waregeshewe mashamba hayo. Jambo lingine ambalo ningependa kulitaja ni kwamba mimi nilipokuwa nikianza uanasheria mwaka wa 1988, niliweza kumtetea Emmanuel Karisa Maitha, ambaye alikuwa kiongozi wa watu wa Pwani. Bw. Karisa Maitha alikuwa akitetea haki za watu wa Pwani na hatimaye, alishikwa na kuwekwa korokoroni Manyani. Nilipata nafasi ya kwenda huko kumuona na alikuwa amefungwa kama mnyama. Mikono na miguu yake yote ilikuwa imefungwa. Alikuwa amewekwa katika chumba kilichokuwa kimejaa maji mpaka kwenye kiuno chake."
}