GET /api/v0.1/hansard/entries/423414/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 423414,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/423414/?format=api",
    "text_counter": 204,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": "Jambo lingine ambalo ningependa kugusia ni juu ya Wakili Rumba Kinuthia. Yeye ni wakili maarufu sana. Lakini ukiona hali yake ya kiafya hivi sasa, ni ya kusikitisha. Yeye ni wakili ambaye nimeangalia hata katika ule uamuzi uliotolewa alipokuwa ameenda kortini, ya kuambiwa kwamba yeye hawezi kupewa ridhaa kwa sababu hakuweza kutoa kithibitisho kuwa aliumia alipokuwa mfungwa korokoroni; kufungwa bila haki na kukosa kuwa na jinsia ya familia yake, kukosa kuwa na mkewe ndani ya nyumba na kwa miaka isiyojulikana kufungiwa korokoroni, hiyo ni haki kweli? Tunasema watu kama hao ambao judgement zao zilikuwa kutupiliwa mbali waweze kuangaliwa. Watu kama Kenneth Matiba, mzee ambaye namjua kwa sababu natoka Pwani na wakati mwingi nimekuwa nikienda South Coast, mzee ambaye alikuwa na afya yake kamili kimwili, ni mtu alikuwa akitembea utamuona kama mtu wa mwili ya kisawa sawa. Hivi leo, ukimwangalia, machozi yanaweza kukudondoka. Yeye ni Mkenya ambaye alisimama kidede akitutetea sisi wengine ambao tuko ndani ya Seneti ili tupate uhuru kama huu. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}