GET /api/v0.1/hansard/entries/423416/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 423416,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/423416/?format=api",
    "text_counter": 206,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Mimi naunga mkono sana Hoja hii. Kuna umuhimu na kwa haraka zaidi kabla mzee wetu, hatusemi mabaya; Mwenyezi Mungu yuko naye, lakini, je, leo akienda mbele ya haki, nani atamlipa kwa aliyopitia? Kwa hivyo, tunasema kwamba ikiwa inawezekana tuweze kutengeneza Compensation Fund ili aweze kulipwa na kuangaliwa hali yake kabla hajaenda mbele zaidi. Pia, ukiangalia kiongozi wa CORD, Raila Amolo Odinga, mtu amefungwa detention mara tatu. Hakuna Mkenya ambaye amefungwa mara tatu isipokuwa yeye. Amepigania uhuru katika nchi hii. Hivi leo hata akiwa anaongea, mimi namuonea huruma. Utaona wakati wote akiwa anaongea mkono wa kushoto unaenda kwenye jicho. Anafuta machozi, yanatoka tu yenyewe hawezi kuyazuia na yeye hajakwenda kortini kusema kwamba anadai lakini watu kama wale ndio wanafaa kuangaliwa. Tukiangalia upande wa makazi, bibi yake mwenyewe, Ida, wakati Raila alipokuwa korokoroni amefungwa bila hatia, bibi yake alifukuzwa kutoka kwa nyumba saa sita za usiku, akiwa na watoto wachanga na akafutwa kazi na Serikali. Ni nani atamlipa Ida Odinga leo? Tunasema kwamba ni lazima kuwe na Compensation Fund kama hii ili waweze kuangaliwa. Mimi naunga Hoja hii ambayo imeletwa na ndugu yangu, Sen. (Dr.) Khalwale. Asante sana."
}