GET /api/v0.1/hansard/entries/424606/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 424606,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/424606/?format=api",
    "text_counter": 453,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": "Asante sana, Bw. Naibu Spika. Kwanza, nataka kumpatia mkono wa heko ndugu yangu, Sen. Moses Masika Wetangula, kwa ushindi wake mkubwa ijapokuwa mimi sikuenda kule kwa sababu nilikuwa mgonjwa. Lakini sio hoja; ushindi wake ulithibitisha kabisa kwamba watu wa Bungoma wanampenda zaidi. Bw. Naibu Spika, Sen. Wetangula amekuwa wakili mkubwa katika nchi hii. Mimi nikiwa kama jaji nimemwangalia katika mikakati zake zote za uwanasheria na pia akiwa Waziri wa Mambo ya Nje. Nafikiri kuwa uamuzi wa ndugu yangu, Sen. Boni Khalwale na Sen. Kennedy Okong’o kujiweka kando na kumpisha ndugu yetu, Sen. Wetangula, kuchukua nafasi hiyo, ni jambo la heko. Bw. Naibu Spika, nampa mkono wa heko na kuunga mkono Hoja hii."
}