GET /api/v0.1/hansard/entries/426178/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 426178,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/426178/?format=api",
"text_counter": 126,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "wa hekima na elimu kuu, huenda nikakataa kidogo kuyakubali mawazo yake kwa sababu kutokwenda shule hakumaanishi kuwa wewe ni mbumbumbu; sio kumaanisha kwamba wewe ni mjinga kupita kiasi. Labda mazingira uliyokuwa ndani yake hayakuwa na nafasi ya kukupa elimu hiyo, hivyo basi ukajipata umekuwa mtu mzima bila kwenda shuleni. Kwa kusoma, haimaanishi kwamba wasoma ili utafute ajira wala kazi ya kusaidia Serikali au kitongoji chako. Sera ya kusoma ni kutafuta nafasi ili ujue na kuelewa mazingira yako yatakayokufaidi wewe na watu wako. Kwa hivyo, vile ninavyoelewa Hoja ya mwalimu Karaba, haikuangaza elimu ya msingi tu. Ametaja elimu ya watu wazima; hakutaja elimu ya watu wazima kwa menajili ya elimu ya msingi tu. Hata nyinyi, Maseneta, mnapotembea hapa na pale mkienda seminaa, huwa mwaenda kutafuta elimu ya watu wazima kwa sababu wengine mko na zaidi ya miaka 18, ambao Katiba ya Kenya inawajumlisha kama watu wazima.Kwa hivyo, sera hizi ninavyozielewa ni kwamba zitakuwa sera ambazo zitaangaza mawazo kutoka kwa elimu ya msingi hadi chuo kikuu, na hata zaidi. Ni wengi ambao wameenda kuchukua shahada ya PhD wakiwa na miaka 60 na zaidi; hiyo ni elimu ya watu wazima. Lakini tunavyoelewa hapa nyumbani, twasema kuwa elimu ya watu wazima ni elimu ya ngumbaru . Ngumbaru maana yake ni kuwaita watu wazima wajinga ama washenzi kwa kukosa kwenda shule, na hili ni kosa kuu. Kwa hivyo, hili neno la elimu ya ngumbaru lafaa liondolewe kabisa; ni neno la matusi kwa umri wa watu hawa ambao hawakupata nafasi ya kupata elimu ya shuleni wakati huo. Sio aibu kukubali kwamba miaka 50 mpaka sasa, kuna wengi wetu ambao hawajaelimika. Lakini jambo la muhimu ni kukubali kwamba wapo wale ambao hawakupata nafasi hiyo; kwa hivyo wapewe nafasi hiyo nao pia wakaangaze mawazo yao na nafasi waliyo nayo sio ya menajili tu ya kujua chakula cha kula, mazoezi watakayofanya au vile Sen. (Prof.) Anyang’Nyong’o amesema wasijitose katika ulimwengu wa kuoa mke wa pili, lakini wawe watu wa kupanua mawazo yao kwa ulimwengu uliopo."
}