GET /api/v0.1/hansard/entries/426188/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 426188,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/426188/?format=api",
    "text_counter": 136,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. (Dr.) Machage",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 179,
        "legal_name": "Wilfred Gisuka Machage",
        "slug": "wilfred-machage"
    },
    "content": "Kwa hivyo, Bw. Naibu Spika, jambo la kuanzisha halmashauri kamili kutekeleza ombi hili la mwalimu Karaba ni jambo la dharura na limepitwa na wakati. Hii ni kwa sababu baadhi ya walimu walioko vijijini ambao wanatekeleza jukumu hili la kuwaelimisha wananchi ambao hawakupata nafasi ya elimu wakati huo ni walevi. Elimu ya wengine wao ni duni na wengine hata hawaendi shuleni na hata vituo hivyo havipo vijijini. Pia, mawazo ya walimu hao hutatanishwa kwa sababu wakati mwingi hata hawana mishahara. Wakati mwingi, sehemu hii ya elimu hata hatambuliki kwa Wizara ya Elimu nchini. Kwa hivyo, ni muhimu kuwa na halmashauri wakati huu na sisi kama viongozi tunafaa kusisitiza jambo hili. Hatufai kuzungumza tu katika Bunge hili bali kuhakikisha kwamba jambo hili limetekelezwa kwa kasi na wakati huu. Bw. Naibu Spika, naunga mkono."
}